Na Rahma Khamis, Maelezo

Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Mhe, Shaaban Ali Othman amesema kuwa lengo la Kuwepo kwa Wizara hiyo ni kuhakikisha kila kijana anakua mzalendo kwa kujenga Uchumi wake na Taifa kwa ujumla

Ameyasema hayo Jang’ombe Wilaya ya Mjini katika Kampeni maalum ya kuwahamasisha vijana kushiriki katika Uchaguzi wa mabaraza yao

Amesema kuwa Wizara imefanya Utafiti na kugundua kuwa ajira zipo hivyo watahakikisha wanaweka mazingira mazuri kwa vijana kupata ajira katika Sekta binafsi pamoja na kubuni ajira nyengine ili waweze kujisaidia

Akizungumzia kuhusu ajira Waziri Shaaban amefahamisha kuwa hakuna ajira ya Serikali ambayo itauzwa kwani kila kijana katika Shehia ana haki ya kupata ajira

Amefahamosha kuwa kuna baadhi ya watu wanauza ajira jambo ambalo ni koaa kisheria na halileti tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla

Aidha amewaasa vijana kuwa tayari kufanya KAZI katika sekta binafsi ili kujiinua kiuchumi

“Pesa zipo muhimu uwe na vigezo ili uweze kuchukua pesa na kujiajiri”alifafanua

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhe, Salama Mbaruok Khatib amewaahidi vijana kuwaunga mkono katika kila hatua ili kuhakikisha wanafaidika kupitia shughuli mbalimbali za kujiajiri na kujipatia kipato

Amesema kuwa Wizara hiyo imeundwa kwa malengo mahsusi ya kuwatafutia vijana ajira hivyo vyema vijana kushiriki katika KAZI mbalimbali

Amesema kuwa Serikali zote mbili zimefanya KAZI kubwa katika kuhakikisha vijana wanajiinua kiuchumi hivyo vyema kila mmoja kuacha kuchagua KAZI ili aweze kunufaika

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha vijana wanashiriki katika shughulinali mbalimbali watatoa mikopo pamoja na kubuni ajira tofauti ili na wao wawe na shughuli za kufanya

Aidha amewataka vijana kwenda katika Shehia kwa ajili ya kuchukua fomu za uongozi na kuwajengea vijana wenzao uwezo kwa ajili ya maslahi yao na Taifa kwa ujumla

  • Kama ni ajira ama fursa zote zitakwenda katika Shehia ili Kila mmoja aweze kupata fursa,tumeamua vijana wote popote walipo lazima wapate ajira” alisisitiza

Hata hivyo awaasa vijana kwa kuacha kuchagua KAZI na badala yake kubadilika ili kuleta maendeleo

Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Ali Haji Hassan amesema kuwa kuanzishwa kwa Baraza hilo Zanzibar kuhakikisha vijana wanasaidiwa na kuunganisha kupitia fursa mbalimbali ikiwemo kiuchumi na kijamii
Aidha

Kwa upande wake Kamishna wa Kinga Tiba na Marekebisho ya Tabia Juma Zidi Kheir amewaasa vijana kutojiungiza katika vitendo viovu vya madawa ya kulevya kwani inapoteza nguvu ya taifa.