Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Kanda ya Ziwa Victoria, Ezekiel Wenje amejiondoa kwenye chama hicho na kujiunga Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wenje ametangaza uamuzi huo mbele ya mkutano mkubwa wa mgombea urais wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Uwanja wa stendi ya zamani ya Muungano leo Oktoba 13,2025.
Wenje amesema hawezi kufanya maandamano hata siku moja.
“Nimecheza Ligi Daraja la Kwanza kwa miaka 15, sasa najiunga na timu ya Ligi Kuu.
“Nilikuwa nasafiri kwa saa nyingi, lakini leo nimetumia saa mbili tu kufika hapa Chato, nimekuja kuunga mkono juhudi hizi kubwa,”amesema.

