Na Peter Haule, JamhuriMedia, Singida

Wizara ya Fedha imeng’ara kwenye Sherehe ya Wafanyakazi (Mei Mosi) Kitaifa, baada ya kuwa mshindi wa kwanza wa mchezo wa mpira wa miguu katika mashindano yaliyoshirikisha Wizara na Taasisi za Serikali.

Tuzo za washindi katika mashindano mbalimbali zimetolewa na Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe za Mei Mosi Kitaifa, zilizofanyika katika Viwanja vya Bombadia Mkoani Singida.

Akizungumza wakati wa maandamano ya wafanyakazi wa Wizara ya Fedha walioshiriki katika sherehe hizo, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Wizara ya Fedha, Bw. Shumbi Mkumbo, alisema kuwa Wizara ya Fedha imenyakua tuzo mbili ikiwemo hiyo ya mshindi wa mpira wa miguu na tuzo ya uendeshaji Baskeli, jambo lililo chochea hamasa kwa watumishi wa Wizara kushiriki zaidi katika michezo.

Alisema kuwa  Wizara itaendelea kuhamasisha michezo kwa kuwa inaimarisha afya kwa watumishi na pia inahimiza umoja na mshikamano.

Sherehe hizo kwa Wizara ya Fedha zimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Naibu Katibu Mkuu, Bi. Jenifa Christian Omolo na Mkurungenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali watu, Bi. Fauzia Nombo.

Katibu wa Hazina Sports Club, Bw.Kelvin Kakoko, akipokea tuzo ya ushindi wa kwanza wa mchezo wa mpira wa miguu kutoka kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) Kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akiwa katika Sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi) Kitaifa, zilizofanyika katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.

Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Fauzia Nombo (kulia), akiwa ameshika moja ya tuzo ambayo Wizara ya fedha imepokea baada ya kushinda mchezo wa mpira wa miguu na kuendesha Baiskeli kwa upande wa Wizara na Taasisi na wakati wa Sherehe za MeiMosi Kitaifa mkoani Singida, kushoto ni Mwandishi Mwendesha Ofisi Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Scholastica Okudo.

Watumishi wa Wizara ya Fedha wakipita mbele ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) zilizofanyika Kitaifa katika viwanja vya Bombadia, mkoani Singida.

Watumishi wa Wizara ya Fedha wakiwa kwenye maandamano wakati wa Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi), zilizofanyika Kitaifa katika viwanja vya Bombadia, mkoani Singida.

Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Fauzia Nombo, akiongoza maandamano ya Watumishi wa Wizara ya Fedha, wakati wa Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi), zilizofanyika Kitaifa katika viwanja vya Bombadia, mkoani Singida.