Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kwamba Ukraine imependekeza kwa Urusi kupitia kwa Marekani mpango wa kusitisha mashambulizi ya pande zote yanayolenga vituo vya nishati.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kwamba Ukraine imependekeza kwa Urusi mpango wa kusitisha mashambulizi ya pande zote yanayolenga vituo vya nishati.
Akitoa hotuba kwa taifa, kiongozi huyo ameweka wazi kwamba ikiwa Urusi iko tayari kusimamisha mashambulizi yake kwenye miundombinu ya nishati ya Ukraine, wao pia watakuwa tayari kufanya hivyo.
Zelensky ameongeza kwamba pendekezo hilo la kusitisha mashambulizi kwenye vituo vya nishati limewasilishwa kwa Urusi kupitia Marekani.
Kutokana na mashambulizi ya Urusi yamekuwa yakilenga vituo vya nishati vya Ukraine, mamilioni ya watu nchini humo huathiriwa na kukosa umeme kwa muda mrefu. Huku Ukraine nayo imekuwa ikilipa kisasi kwa kulenga vituo vya mafuta vya Urusi ambavyo ni tegemeo la kiuchumi la Urusi.


