Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema leo kwamba malengo yake juu ya mkutano kati ya Marekani na Urusi kuhusu vita nchini mwake ni kwa Urusi kuacha kuwaua Waukraine na kukubali kusitishwa kwa mapigano.

Zelensky ambaye mapema leo aliweka wazi utayari wake wa kukutana na rais Putin ameyasema hayo katika chapisho lake aliloliweka katika mtandao wa kijamii wa X na kuongeza kwamba mkutano huo uwe na dhamira ya kweli ya kutafuta amani ya kudumu.

Katika hatua nyingine, Rais wa Urusi Vladmir Putin amegusia juu ya uwezekano wa kufanya mkutano na Zelensky na kusema kwamba hana kipingamizi ingawa lazima kuwe na masharti ya mazungumzo hayo.

“Nimesema mara kwa mara kwamba sina pingamizi lolote dhidi ya fursa hii ya mkutano na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, lakini masharti fulani yanapaswa kutayarishwa katika hili. Cha kusikitisha ni kwamba, tuko mbali kabisa katika kutengeneza mazingira kama hayo.” amesema Putin.