MKANDARASI WA KITUO CHA AFYA GAIRO ATAKIWA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameutaka uongozi wa wilaya ya Gairo unamsimamia mkandarasi na kuhakikisha upanuzi wa kituo cha afya na unakwisha kwa wakati.
Akizungumza na uongozi na mkandarasi wakati wa ziara yake mwishoni mwa wiki iliyopita ya kukagua maendeleo ya Wilaya ya Gairo, Mhe. Kebwe amesema kuwa hajaridhishwa na kasi wanayokwenda nayo katika upanuzi wa kituo cha afya unaofanyika hivi sasa licha ya kuwa fedha za kituo hizo zote zimeshatolewa.
 “Ni nini kinakwamisha ujenzi kuisha wakati fedha mmeshapewa???? amemuuliza Mkandarasi na Uongozi unaosimamia jengo hilo … nawaomba sana, hebu fanyeni haraka maana kuna baadhi ya huduma wananchi wanakwenda kuzipatia mbali,” amesema.
Amesema kuwa ipo haja ya kila mtu kutimiza majukumu yake bila ya kusukumwa sukumwa maana hali ya sasa ni kazi tu. Awali akitoa maelezo ya ujenzi, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Dennis Ngaromba amesema kuwa ujenzi huo umeshagharimu zaidi ya milioni 139 na baada ya kukamilika jumla ya wananchi wapatao 218,000 wataweza kupatiwa huduma huku vipimo vyote vikipatikana.
“Kituo hiki cha afya kitakuwa ni cha kisasa na kitakuwa na vipimo vyote huku huduma zote zikipatikana maana kimekaa pembezoni mwa barabara ya Gairo-Dodoma,” amesema.
Upande wake Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe kwa kuweza kutembelea wilaya yao na kuhamasisha wananchi kuendelea kujitoa katika shughuli za maendeleo.
Mhe. Mchembe amewashukuru wananchi kwa kuendelea kujitolea katika shughuli za maendeleo ya wilaya yao na kuwaomba kuwa bega kwa bega kuwafichua wale wote wanaokwamisha shughuli za maendeleo.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (aliyeshika tofali na mwiko) na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Rachel Nyangasi (wa kwanza kulia) wakishirikiana kujenga ukuta wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (aliyebeba tofali) kumsaidia fundi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe kujenga ukuta wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akikagua ujenzi kwa ajili ya kupanua eneo la kulaza, na sehemu ya kuhifadhia maiti wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akishiriki katika ujenzi wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (wa kwanza kushoto) wakati akikagua upanuzi wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Dennis Ngaromba (wa kwanza kulia) wakati akitoa maelezo juu ya upanuzi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakiangalia mchanganyo wa saruji na mchanga.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) akipima ukuta kuona kama wamefikia viwango vinavyotakiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Dennis Ngaromba (wa kwanza kulia) wakati akitoa maelezo juu ya ujenzi wa jengo ya kuhifadhi maiti.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakiwa mbele ya jengo jipya la kuhifadhi maiti.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakikagua kijengo kidogo kilichokuwa kikitumika miaka ya nyuma kuhifadhia maiti.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakiwa mbele ya jengo la zamani la kuhifadhi maiti.