Daily Archives: May 14, 2019

Wamdanganya Magufuli

Kashfa imegubika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wafanyakazi, Mei Mosi mwaka huu yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya. Kashfa hiyo imekikumba Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU). Ndani ya chama hicho, baadhi ya viongozi wake wanadaiwa kuwasilisha jina la kigogo asiyestahili kuwa mfanyakazi bora, akapewa mkono na Rais Dk. John Magufuli na kukabidhiwa cheti cha mfanyakazi bora na zawadi ya ...

Read More »

Aibu barabara za ‘City Center’ Dar

Mvua zimekuwa jambo la kutia aibu katika Jiji la Dar es Salaam. Kwa wengi jijini Dar es Salaam, kama ni suala la kuchagua kati ya mvua na jua ili kutunza aibu ya uongozi wa jiji hilo, basi ni afadhali kuvumilia joto la kiangazi kuliko mvua za wakati wa msimu wa masika. Mvua zimekuwa zikiumbua udhaifu wa viongozi wa Jiji la ...

Read More »

Bodaboda ahofiwa kufia Polisi

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linatuhumiwa kumuua kwa kipigo dereva wa bodaboda, Josephat Jerome Hans, baada ya kumtuhumu kwa wizi wa kompyuta mpakato (Laptop) katika nyumba ya kulala wageni ya Blue Sky jijini humo. Tuhuma hizo zimo kwenye barua ya mama mzazi wa kijana huyo, Lusina Joseph Kiria, aliyomwandikia Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mwezi ...

Read More »

Fedha za wastaafu zakwapuliwa

Shilingi bilioni 1.2 zikiwa ni fedha za malipo ya mafao ya walimu wastaafu katika Mkoa wa Mara zinadaiwa kukwapuliwa na mafisadi, Gazeti la JAMHURI linaripoti. Mamilioni hayo ya fedha yameelezwa kuchukuliwa kupitia njia ovu ya mikopo hewa. Baadhi ya viongozi wa serikali wanaosimamia masilahi ya watumishi wanahusishwa na tuhuma hizi. Wanadaiwa kushirikiana na baadhi ya wafanyabiashara kufanikisha mchezo huo. Waathirika ...

Read More »

Dengue mtihani

Si kila homa ni malaria! Kauli hii inapaswa kuzingatiwa hasa kipindi hiki ambacho ugonjwa wa homa ya dengue unatajwa kushika kasi jijini Dar es Salaam. Serikali imethibitisha ugonjwa huo kusambaa kwa haraka katika wilaya za Ilala, Kinondoni na Ubungo. Kutokana na hali hiyo, wakazi wa maeneo hayo wametakiwa kuwahi katika vituo vya afya ama hospitalini wanapohisi mabadiliko katika miili yao ...

Read More »

Waziri Mkuu apigwa yai

Waandamanaji wamempiga kwa yai Waziri Mkuu wa Australia, Scott Morrison. Mkasa huo dhidi ya waziri mkuu ulitokea wakati wa mkutano wa kampeni Jumanne wiki iliyopita, bila kusita, walimtandika yai la kichwa. Vipande vya video vya tukio hilo vilionyeshwa kwenye televisheni za nchi hiyo. Walinzi wa waziri mkuu huyo mara baada ya kitendo hicho, haraka sana, wakamdaka mwanamke mmoja miongoni mwa ...

Read More »

Marais wataka uuzaji pembe za tembo

Nchi tano za kusini mwa Afrika zenye idadi kubwa ya tembo zimeanza kudai haki ya kuuza pembe za wanyama hao kwa msisitizo kuwa rasilimali hiyo iwekewe utaratibu utakaonufaisha wakazi wa maeneo ya mapori wanamohifadhiwa. Marais kutoka nchi za Botswana, Zimbabwe, Zambia na Namibia, pamoja na Waziri wa Mazingira kutoka Angola walikutana wiki iliyopita mjini Kasane, Botswana, kuweka sera ya pamoja ...

Read More »

Nigeria kutoa rais wa UNGA

Baada ya miaka 30 kupita Nigeria inaweza kutoa rais wa Baraza la Umoja wa Mataifa (UNGA). Kwa mara ya mwisho Joseph Nanven Garba ndiye aliyekuwa Rais wa UNGA mwaka 1989 kutoka Nigeria. Profesa Tijjani Muhammad Bande ambaye kwa sasa ni mwakilishi wa kudumu wa Nigeria katika Umoja wa Mataifa, ndiye anatarajiwa kushika urais wa UNGA kutoka kwa rais wa sasa, ...

Read More »

Mambo 6 kutoka kwa Mengi

Habari mpendwa msomaji. Kwanza kabisa niombe radhi kwa kutoendelea na makala ya ‘Nina Ndoto.’ Makala hizi zitaendelea kama kawaida wiki ijayo. Mapema Alhamisi ya wiki mbili zilizopita ilikuwa asubuhi yenye majonzi kwa Watanzania wengi. Tuliondokewa na mpendwa wetu Dk. Reginald Abraham Mengi. Mengi amekuwa mtu aliyegusa maisha ya watu wengi ndiyo maana nikaona si vema kuacha jambo hili lipite tu ...

Read More »

Haki itendeke katika hili

Moja ya habari zilizochapishwa na gazeti hili ni kuhusu kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa mtuhumiwa wa uhalifu, Josephat Jerome Hans, akiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma. Habari hiyo imeeleza kuwa kijana huyo anatuhumiwa kwa wizi wa Laptop katika moja ya nyumba za kulala wageni Dodoma. Tayari mama mzazi wa mtuhumiwa huyo, Lusina Joseph Kiria, ameandika malalamiko yake ...

Read More »

Ujamaa… (46)

Katika maisha ya Kiafrika ya kizamani watu wote walikuwa sawa. Walishirikiana pamoja na walishiriki katika uamuzi wowote unaohusu maisha yao. Lakini usawa huu ulikuwa usawa wa kimaskini; ushirikiano wenyewe ulikuwa wa vitu vidogo vidogo. Na serikali yao ilikuwa serikali ya jamaa, au ukoo, na ikizidi sana labda ya kabila zima. Kwa hiyo kazi yetu ya sasa ni kuibadilisha kidogo hali ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (13)

Wiki iliyopita nilisitisha safu hii kwa toleo moja kwa nia ya kuandika juu ya kifo cha mmiliki wa vyombo vya habari, Dk. Reginald Mengi. Hadi leo bado naendelea kusikitika na Watanzania wanasikitika. Hata hivyo, ni lazima maisha yaendelee. Tumwombee huko aliko apumzike kwa amani, ilhali sisi tuliobaki tukiendelea kumuenzi kwa kazi ya mfano aliyoifanya maishani mwake. Sitanii, safu hii inasema: ...

Read More »

Ndugu Rais kinywa kiliponza kichwa

Ndugu Rais, kinywa kilikiponza kichwa ni maneno yenye hekima yaliyosemwa na wahenga wetu. Jikwae sehemu yoyote, lakini usijikwae ulimi. Maneno yakishamtoka mtu hawezi kuyarudisha mdomoni. Sijui wanakuwa na maana gani wanaosema futa maneno yako. Maneno yaliyokwisha tamkwa hayawezi kufutwa wala kufutika. Eti iwe kama vile hayakutamkwa. Haiwezekani. Unachoweza kufanya ni kutamka maneno mengine ya kupooza yale yaliyokwisha tamkwa. Hii tumeona ...

Read More »

‘Mmasai wa kwanza kupiga dansi’ (3)

Wimbo mwingine uliotia fora wakati huo ni ‘Bide’, alitunga na kuimba kwa lugha ya Kipogoro. Juma Ubao aliamua kupumzika mambo ya muziki kwa kipindi kifupi. Atumia muda huo wa mapumziko kwenda kusoma  masomo ya jioni akiwa na lengo la kuendeleza elimu yake. Alisoma masomo ya Uhasibu na Biashara ambako aliweza kupata cheti. Cheti chake kilimpa nafasi ya kupata ajira katika ...

Read More »

Wapinzani wa Messi dhidi ya Simba SC

Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa imezidi kuinogesha Tanzania katika ulimwengu wa soka kiasi cha kuongeza ushindani miongoni mwa timu kubwa hapa nchini. Hii ni kampuni ya michezo ya kubahatisha ambayo imepata kutoa udhamini kwa timu kadhaa hapa nchini, ambazo ni pamoja na Yanga, Simba, Mbao na Singida United. Safari hii, miongoni mwa timu hizo kubwa zilizopata kuwa chini ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons