Monthly Archives: August 2019

Hotuba ya Rais uzinduzi wa Terminal III Uwanja wa JNIA Agosti 1, 2019

Rais Magufuli: Watanzania tukatae kuitwa maskini Ndugu zangu, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha leo hapa tukiwa wazima na wenye siha njema. Pia namshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi kwa kunialika kwenye hafla hii ya uzinduzi wa jengo la tatu la abiria ‘Terminal III’ katika Kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Jengo hili ni la kisasa kuliko ...

Read More »

TPA: Bandari ya Mtwara ni fursa mpya kwa nchi za SADC

Katika makala hii tunakuletea maelezo kuhusu Bandari ya Mtwara, ambayo ni miongoni mwa bandari za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ambazo zipo kimkakati katika kuhudumia soko la nchi za SADC.  Bandari hii ya Mtwara inasimamia bandari ndogo ndogo za Lindi na Kilwa. Kutokana na mikakati mbalimbali inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais wa ...

Read More »

Ndugu Rais tuandalie meza ya maridhiano

Ndugu Rais, tumtangulize Muumba wetu kwa kuwashukuru wachungaji na mapadri wa Dodoma ambao kwa wakati wote wamekuwa wakiniombea uzima wawapo katika sala zao! Nimeisikia sauti yenu na baba yenu wa mbinguni anazipokea sala zenu. Mwenyezi awabariki ili siku moja mje muishuhudie tena amani ya kweli katika nchi yenu hii mliyopewa na Muumba wenu kwa neema tu! Nchi yenye upendo, umoja ...

Read More »

Barua ya wazi kwa Rais John Magufuli

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mimi ni mahabusu ambaye nimo gerezani kwa amri ya mahakama nikituhumiwa kesi ya kubambikiwa ya mauaji. Nimo gerezani tangu Mei 08, 2016 mpaka hivi sasa unavyosoma barua hii. Mheshimiwa Rais, sababu ya kupewa kesi hii ni kutokana na askari polisi wa Kituo cha Usa-River [jina limehifadhiwa] ambaye kwa sasa ameamua kuishi na mke ...

Read More »

Mfumo wa Tehama kuzilinda barabara

Bodi ya Mfuko wa Barabara imo mbioni kuzindua mfumo wa Teknolojia na Mawasiliano (Tehama) utakaowashirikisha wananchi katika kufuatilia uharibifu na matengenezo ya barabara. Lengo la kuanzishwa kwa mfumo huo ni kuwawezesha na kuwashirikisha watumiaji wa barabara kutoa taarifa kwa mamlaka husika juu ya uharibifu wa miundombinu hiyo. Hayo yamesemwa na Eliud Nyauhenga, Meneja wa Mfuko wa Barabara wakati wa kilele ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (40)

Unapotaka kufanikiwa, uwe kama udongo mikononi mwa mfinyanzi Unyenyekevu ni mtihani. Unapojivuna kuwa umeupata unyenyekevu unapotea. Kama wewe ni mnyenyekevu usiwaambie watu kuwa wewe ni mnyenyekevu. “Kuanguka hakuumizi wale ambao wanapaa chini chini.” (Methali ya China). Ukipaa juu sana unapoanguka unaumia sana. Wanyenyekevu wanapaa chini chini. Unyenyekevu na kujiamini ni pande mbili za sarafu moja. Kwangu mimi, unyenyekevu na kujiamini ...

Read More »

Mchawi wa ajira tunaye wenyewe

Serikali imetenga Sh bilioni 40 kwa mwaka huu wa fedha wa 2019/2020 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo vya VETA katika wilaya 25 nchini. VETA wanasema maombi ya vijana wanaotaka kujiunga kwenye vyuo vyake yamefikia 800,000 kwa mwaka ilhali uwezo ilionao ni wanafunzi 200,000 pekee! Hii ina maana robo tatu ya vijana wanakosa nafasi! Makisio ya VETA ni kuhakikisha inapokea ...

Read More »

Nia njema tabibu, nia mbaya harabu

Nia ni kusudio, yaani dhamiri ya kutaka kukamilisha jambo au haja. Binadamu hafanyi jambo bila ya kuwa na nia katika nafsi yake. Nafsi humsukuma kutaka jambo lake lifanikiwe katika umbo la uzuri au ubaya. Nia nzuri au mbaya huonekana binadamu anapoonyesha dhamiri yake kwa binadamu wenzake. Nia njema hupokewa kwa shangwe na nia mbaya hupokewa kwa masikitiko.  Ndipo Waswahili tunaposema, ...

Read More »

Yah: Siasa ni muhimu kwa taifa lolote

Naanza na salamu. Salamu ni uungwana wa kawaida kwa muungwana yeyote ili aweze kuwasiliana na mwenzake, maisha ya kuishi kila mtu akimuona mwenzake ni adui si maisha mazuri na kupishana kwa itikadi hakutufanyi tuwe maadui na kukubali matokeo ya walio wengi ni jambo la busara katika ulimwengu wa siasa za ushindani. Nimeamua leo kumaliza barua yangu mapema sana kabla ya ...

Read More »

Gamboshi: Mwisho wa dunia (9)

Wiki iliyopita katika sehemu ya 8 hadithi hii iliishia katika aya inayosema: “Shahidi wa pili alikuwa Bibi Judith mwenyewe. Aliieleza mahakama jinsi siku moja walivyokuja jamaa watatu. Mmoja alikuwa Mzungu, mwingine Mwarabu na wa mwisho alikuwa mtu mweusi Mwafrika. Watu hawa alidai mama huyu kuwa eti walimuomba ajiunge katika shughuli zao za kichawi. Lakini mama huyu eti alikataa kata kata. ...

Read More »

Fid Q kusherehekea ‘birthday’ na Kitaaolojia

Msanii wa muziki wa hip-hop, Farid Kubanda, maarufu kama Fid Q, kila ifikapo Agosti 13, husherehekea siku yake ya kuzaliwa. Mashabiki wa muziki wa Fid Q wanafahamu Agosti 13 hufanya nini kwa mashabiki wake. Fid Q hutumia fursa hiyo kukonga nyoyo za mashabiki wake kwa kuachia wimbo mpya ambao ndani yake hudhihirisha kila mwaka kwamba yeye ni mwamba wa hip-hop nchini. Fid ...

Read More »

Mashabiki Simba, Yanga tatizo

Kila wakati uteuzi wa wachezaji wa Taifa Stars umekuwa ukiambatana na malalamiko ya mashabiki wa Simba na Yanga. Kocha yeyote yule atakayechagua timu ya taifa, lazima atajikuta akiangukia kwenye uadui na mashabiki wa Simba au wale wa Yanga. Wachezaji wa Yanga wakiwa wengi uwanjani, mashabiki wa Simba wataishangilia Taifa Stars kwa shingo upande. Hali huwa hivyo hivyo ikiwa wachezaji wa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons