Author Archives: Jamhuri

Haya Hapa Magazeti ya Leo Januari 26, 2018

Kama upo mbali na meza za magazeti mtaani kwako basi husipitwe na kilichoandikwa kwenye magazeti ya leo Ijumaa Januari,26, 2018 nimekuekea hapa

Read More »

WEMA: Jamaani Kule Nimeshindwa Sasa Narudi Nyumbani

“Siwezi Kuendelea kuishi kwenye Nyumba inayo nikosesha amani… Peace of mind is everything for me… Natangaza Rasmi kuondoka Chadema na Kurudi Nyumbani.” Maneno hayo yameandikwa na muigizaji Wema Sepetu kupitia ukurasa wake wa Instagram akitangaza uamuzi wake wa kuhama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM). Wema Sepetu ametangaza uamuzi huo ikiwa ni meizi 10 ...

Read More »

Zaidi ya Million 20 Zapatikana Kusaidia Watoto Wenye Ulemavu

Zaidi ya milioni 20 zimetolewa na wananchi pamoja na Taasisi mbalimbali hapa  nchini ikiwa ni mchango wa kusaidia matibabu na kununua vifaa tiba kwa ajili ya  watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi. Ikiwa Jana ni Jumanne ya kutoa (GIVING TUESDAY) kote duniani na Taasisi ya Foundation for Civil Society iliadhimisha kwa kuwasaidia watoto hawa kwa kuwapatia vitu hivyo,huku kauli ...

Read More »

LHRC Yabaini Mapungufu Kibao Uchaguzi wa Madiwani

  MKURUGENZI wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga, amesema kuwa kituo hicho kimefuatilia kwa ukaribu uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 ulifanyika Novemba 26 mwaka huu, katika halmashauri 36 kwenye mikoa 19 nchini. Katika uchaguzi huo tume ya haki za binadamu imebaini matukio mbalimbali ya uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu, vikiwemo vitendo vya ...

Read More »

TCU, mustakabali wa elimu Tanzania (2)

Na Mwandishi Wetu, Arusha Katika makala iliyotangulia nilifafanua gharama ya uamuzi wa TCU kwa upande mmoja kuzuia baadhi ya vyuo binafsi, kati yake vimo vile vinavyomilikiwa na taasisi za dini, kutodahili wanafunzi kwa mwaka huu wa masomo na kuzuia baadhi ya kozi zisiendelee kufundishwa. Tafsiri ya uamuzi huu ni kama vile, leo taasisi binafsi ndiyo chanzo cha kudorora kwa elimu ...

Read More »

Mama yetu ni mmoja Tanzania

Ndugu Rais  na wana wote wa nchi hii mama yetu ni mmoja tu, naye ni mama Tanzania. Nchi yangu kwanza, umoja na mshikamano katika mama huyu ndiyo mwamba wetu. Maandiko yanasema mwenye busara na hekima akitaka kujenga nyumba, hujenga nyumba yake juu ya mwamba ili hata mvua na upepo zikivuma, nyumba haitetereki. Bali amekosa busara na hekima mtu yule ambaye ...

Read More »

Kipofu amshonea shati Rais Kikwete

Siku ya Jumatatu, saa 6:00 mchana nimeikamilisha safari yangu ya kwenda nyumbani kwa Dk. Abdala Nyangaliyo, anayeishi Mbagala Kibondemaji A, jijini Dar es Salaam Dk. Nyangaliyo ni maarufu na hata cheo cha udaktari amepewa tu kwa heshima, lakini siyo kwamba alikisomea. Umaarufu wa Dk. Nyangaliyo unatokana na ulemavu alionao wa kutoona (kipofu), lakini anafanya kazi ya kushona nguo na kufundisha ...

Read More »

Kuna maisha baada ya maisha

Jumapili Februari 12, 2017 saa 4:00 za usiku nilipokea taarifa kifo cha baba yangu mzazi kutoka kwa kaka yangu mkubwa aitwaye John. Ohooooo!, nilishikwa na butwaa iliyoandamana na huzuni, sikuamini. Moyo wangu haukuamini, akili yangu iliukataa ukweli kuondokewa na baba mzazi, Raphael Bhoke. Hii yote ni kutokana na ubinadamu wangu, binadamu tumeumbwa kutokubali kupoteza bali kupokea tu. Nilichukua kitabu cha Norman ...

Read More »

 Serikali ikiwa mbaya, CCM itakuwaje nzuri?

Vinara wawili, kati ya wale wanaotuhumiwa kuifanya Loliondo isitawalike, wamewatumia wanasheria wao kuniandikia barua wakitaka ‘nisiwaguse’ kwa chochote kinachoendelea Loliondo. Edward Porokwa na Maanda Ngoitiko, wanaamini kwa kuninyamazisha mimi na Gazeti la JAMHURI, ‘sifa na utukufu’ wao katika Loliondo, vitaendelea kudumu! Maandishi ya wanasheria wao yameandikwa kwa lugha ya mbwembwe nyingi, lakini sikuona mahali walipokanusha yaliyoandikwa juu ya Loliondo na ...

Read More »

Haya ndiyo mambo madogo unayoweza kuyafanya na yakakuletea manufaa makubwa kwenye afya yako

Mara nyingi tumekuwa tukidharau mambo madogo madogo sana ambayo yapo ndani ya uwezo wetu kuyatekeleza ambayo kupitia hayo, tungeweza kuzinufaisha afya zetu kwa kiasi kikubwa sana na kujiepusha na magonjwa hasa yasiyo ya kuambukiza. Wengi wetu tumejikuta tukipata maradhi mbali mbali na kulazimika kubeba mzigo mkubwa wa matibabu, lakini huenda kinga yake ni kufuata tu masharti madogo madogo sana ya ...

Read More »

Tetesi za usajili Ulaya

Baada ya kukamilika kwa usajili wa Neymar kutoka Barcelona kwenda PSG, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Javier Pastore, amempa Neymar  jezi  namba 10 akisema ni shukrani yake kwake ajisikie kuwa nyumbani (tovuti ya PSG). Naye Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane, anaamini kuwa klabu yake lazima imuuze Gareth Bale (28), kama inataka kumsajili Kylian Mbappe, mwenye umri wa miaka 18, ...

Read More »

Michezo chanzo kikuu ajira

NA MICHAEL SARUNGI Serikali inaandaa mikakati mahsusi ya kuhakikisha sekta ya michezo nchini inakuwa moja ya vyanzo vya ajira na mapato kwa vijana. Akizungumza na JAMHURI baada ya kukabidhi bendera kwa Timu ya Taifa ya Riadha inayoshiriki mashindano ya riadha ya dunia nchini Uingereza, yatakayofanyika kuanzia Agosti 4 hadi 13, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ...

Read More »

Magufuli awanyoosha

*Sasa aanza kutumbua mawakala wa ushuru *MaxMalipo na wenzake awapeperushia njiwa   NA MICHAEL SARUNGI   Baada ya kuwanyoosha watumishi wa umma wa Serikali Kuu, Rais John Magufuli sasa ameingia kwenye “ushoroba” wa wazabuni, ambao wamekuwa wakipata malipo yasiyolinga na kazi wanayofanya, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. Fagio la Rais Magufuli sasa limeanza kuzikumba kampuni zilizokuwa zinatoa huduma ya kukusanya ushuru ...

Read More »

CUF wabemenda demokrasia

Na Thobias Mwanakatwe   MGOGORO wa kiasiasa unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) umedhihiriha jinsi viongozi wanavyofinyanga sharia na demokrasia ya vyama vingi ilivyo na mwendo mrefu kabla ya kufikiwa. Chama hicho ambacho ni cha tatu kwa ukubwa nchini, mgogoro wake ulianza baada ya Prof. Ibrahimu Lipumba kujizulu nafasi ya uenyekiti wa taifa wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba ...

Read More »

Lipumba anachoma nyumba aliyomo!

Naandika makala hii nikiwa hapa jijini Tanga. Nashiriki mkatano wa mwaka wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na wanahabari. Nimepata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Msitu wa Amani. Msitu huu ulioko Muheza ni wa aina yake. Msitu uko kwenye bonde na kingo za milima. Msitu umehifadhiwa na unayo miti iliyokomaa usipime. Miti hii inakua, inazeena na kuanguka au kuangushwa ...

Read More »

Ijue teknolojia ya kufundisha kusoma

GraphoGame (GG) au GrafoGemu kwa Kiswahili, ni mchezo unaotumia teknolojia rahisi ambao ulibuniwa na timu ya utafiti ya Chuo Kikuu cha Jyvaskyla cha nchini Finland chini ya usimamizi na uongozi wa Profesa Heikki Lyytinen. Japokuwa mchezo wa GrafoGemu ulianza katika lugha ya Kifini (ukiitwa Ekapeli), hadi sasa mchezo huu umeweza kutengenezwa katika lugha mbalimbali kama vile Kiingereza, Kispaniola, Kijerumani, Kiswidi, ...

Read More »

TCU itulie, isichezee elimu

Na Mwandishi Maalum, Arusha   Kwa wiki yote iliyopita habari iliyogusa wengi katika sekta ya elimu ni ile iliyohusu kuzuiwa kwa vyuo 19 vinavyotoa elimu ya juu (vyuo vikuu) na baadhi ya vyuo kuzuiliwa kudahili wanafunzi katika baadhi ya kozi wanazotoa. Jambo hili limegusa watu wengi, wazazi na walezi, wanafunzi na walimu wa vyuo husika. Uamuzi huu kutoka Tume ya ...

Read More »

Utapeli wa viwanja balaa Moshi

MOSHI    CHARLES NDAGULLA Eneo la Njiapanda katika Mji Mdogo wa Himo, mkoani Kilimanjaro linalosifika kuwa kitovu cha biashara ya magendo, hasa mahindi, yanayosafrishwa kwenda nje ya nchi kwa njia za panya, sasa limeongezewa sifa nyingine.   Sifa hii ya pili ni utapeli wa viwanja unaosimamiwa na watendaji wa serikali akiwamo Afisa Mtendaji wa Kata ya Njiapanda, Humphrey Kimath ambaye ...

Read More »

Hisia ovu za kishirikina zinavyosumbua jamii Bukoba Vijijini

Na Prudence Karugendo   KAMULI ni kijiji kilichomo Kata ya Kibilizi, Tarafa ya Rubale,  Bukoba Vijini, mkoani Kagera. Kwenye kijiji hicho kumejitokeza hisia na imani za kishirikina ambazo zimeanza kuwafanya wananchi kukosa amani na kuanza kuishi kwa mashaka makubwa kwa kila mwanakijiji kushindwa kuelewa ataionaje kesho!   Mwaka 2015, bibi mmoja mwenye umri wa miaka 80, Florida Anatori, pamoja na ...

Read More »

Ngeleja: Escrow haijaniyumbisha

Na Thobias Mwanakatwe   JINA la William Mganga Ngeleja lilianza kufahamika zaidi ndani na nje ya nchi mara tu baada ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2005 katika Jimbo la Sengerema, mkoani Geita na kuwashinda wagombea wenzake saba katika mchakato wa kura za maoni. Ngeleja ambaye hadi sasa bado ni mbunge wa jimbo hilo ikiwa ni kipindi ...

Read More »

Lugha isivunje nguzo zetu za Taifa

Na Angalieni Mpendu Lugha yoyote ni chombo cha lazima kwa mawasiliano na uelewano kati ya wanadamu. Lugha ikitumika vizuri na kwa ufasaha katika kundi moja na jingine au Taifa moja na taifa jingine huleta tija, maendeleo na uhusiano mwema. Ikitumika vibaya hujenga chuki na mifarakano. Unapoitathmini lugha katika matumizi mazuri huneemesha hekima, hujenga umoja na hudumisha amani, kuanzia familia hadi ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons