Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli. Mimi ambaye ni mkazi wa Mkoa wa Tabora niliporwa nyumba yangu mwaka 2006 na wenye uwezo wa kiuchumi lakini mpaka leo sijafanikiwa kuipata.

Kwamba mheshimiwa rais, nilijitahidi kufuata hatua zote muhimu zikiwa ni pamoja na za kijamii na za kisheria ndani ya mkoa huu ilishindikana.

Kwamba mheshimiwa rais, kutokana na hali ya mambo kuwa kama nilivyojieleza hapo juu, nimeamua kulifikisha suala hili kwako kwa ufumbuzi.

Kwamba mheshimiwa rais, imani yangu kwako kuhusu suala hili ina misingi kwani masuala mengi yakiwemo na ya ardhi, ambayo yalishindikana kutatuliwa na viongozi wa chini yako, wewe ulipoletewa uliweza kutatua.

Kwamba mheshimiwa rais, najua unayo majukumu mengi kwa taifa name nakuomba unipokee kwani wewe ni baba wa watu wote wa taifa hili na mimi nikiwa miongoni mwa watoto wako na hasa ningeshukuru kama ningepata nafasi ya kukuona ana kwa ana nawe ili niweze kukueleza kwa kirefu jinsi tatizo langu lilivyo.

Wako mtiifu

Singu Samike – Tabora 0767-189130

1590 Total Views 2 Views Today
||||| 2 I Like It! |||||
Sambaza!