Mheshimiwa Rais Jakaya M. Kikwete, kwa unyenyekevu na heshima ninaleta ombi la kuonana nawe ana kwa ana nikueleze shida inayonikabili.

Mheshimiwa Rais, utakumbuka mwaka 2008 Mhe. hayati Mzee Rashid M. Kawawa alileta kwako ambi maalumu linalonihusu mimi Bi Bernadette Bernard Mulokozi pamoja na baadhi ya watu waliokuwa na matatizo tofauti wakiwamo walioonewa na Mahakama.

 

Mama Zainabu Mkwawa na wengine kati yetu walitimiziwa haja zao, lakini mimi hadi hivi leo sijapata msaada zaidi ya kuzuiwa mlangoni kwako na kuwekewa vikwazo.

 

Nimejaribu kuwasiliana nawe kwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS) bila mafanikio. Pia nilitafuta njia mbadala, nikajaribu kuja nyumbani kwako nikawekewa vikwazo.

 

Nilipata kuleta barua nikawapatia wasaidizi wako lakini sijasaidiwa, sijui kama ilikufikia.

Nilijaribu kwenda kwa Waziri Mkuu, nilipofika nyumbani kwake nikazuiwa kuingia.

 

Mheshimiwa Rais, nimejaribu pia kuwasiliana na familia ya Mwalimu Julius Nyerere, mawaziri na wabunge mbalimbali akiwamo Stephen Wasira, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Mshitaka (DCI), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na maofisa wa haki za binadamu ili wanaisaidie kufikisha ujumbe wangu kwako, lakini bado sijapata msaada wowote.

 

Nilishafikisha tatizo lango kwa idara yako ya mawasiliano, katibu wao na Katibu Mkuu Kiongozi.

 

Kwa sasa niko katika hatari ya kunyang’anywa ‘kizimba’ kwa sababu sijakilipia, na nina sikitika kwani inaonekana kama vile kuna visasi vya ndani kwa ndani.

 

Hivyo kwa barua hii ya wazi, ninaomba kuonana na wewe Rais Jakaya M. Kikwete nikuelezee taabu yangu.

 

Ndimi mwanao mtiifu,


Bernadette B. M Mlokozi

Simu: 0688116792

1575 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!