Watu wanne wamefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa ambapo watano kati yao hali zao ni mbaya baada ya kutokea ajali ya basi la Kampuni ya Arusha Express lenye namba za usajili T 750 BYQ katika eneo la Bonga, Babati mkoani Manyara leo Jumatatu, Oktoba 8, 2018.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Augustino Senga amesema basi hilo la kampuni ya Arusha Express lilikuwa likitokea Arusha kuelekea Mbeya na kwamba watu watatu walifariki papo hapo na mmoja alifariki wakati akipelekwa hospitali kwa matibabu.

 

Amesema Polisi wanaendelea kuchunguza chanzo cha ajali huku wakimtafuta dereva ambaye amekimbia baada ya ajali.

1109 Total Views 3 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!