Mbunge wa Uganda anayedaiwa kupigwa na wanajeshi ameruhusiwa kuondoka nchini humo , kulingana na maafisa wa polisi

Hatua hiyo inajiri kufuatia madai kwamba mbunge huyo alipigwa mara kadhaa akiwa katika kizuizi cha jeshi, madai ambayo yamekataliwa na jeshi.

Yeye na wanasiasa 32 wa upinzani walishtakiwa na shtaka la uhaini wiki iliopita kufautia madai ya kuupiga mawe msafara wa rais Yoweri Museveni.

Bobi Wine mapema aliachiliwa kwa dhamana lakini akaambiwa kwamba hawezi kuondoka Uganda.

Siku ya Ijumaa , maafisa wa polisi walithibitisha kwamba alikuwa ameruhusiwa kuondoka nchini humo kwa matibabu maalum baada ya serikali kutuma kikosi cha madaktari tisa kumchunguza hali yake.

Wakili wa Bobi Wine mapema alikuwa amesema kuwa mwanamuziki huyo alikuwa amekamatwa kwa nguvu akiwa katika uwanja wa ndege siku ya Alhamisi, ijapokuwa jaji alikuwa amemruhusu kupata pasipoti yake kwa sababu alihitaji kuondoka nchini humo kwa sababu za kimatibabu.

Alikamatwa kwa nguvu na kutupwa katika ambalensi ya ya polisi.

Msemaji wa polisi alisema katika ujumbe wake wa Twitter kwamba Bobi Wine alikuwa akifanyiwa uchunguzi kutokana na madai ya kupigwa.

Pia walisema kuwa mbunge mwengine wa upinzani Francis Zaake alikuwa akijaribu kuelekea Ulaya kwa matibabu , alikuwa akijaribu kutoka Uganda lakini akakamatwa.

Wakati huohuo wafuasi wa Bobi Wine wamefanya maandamano katika mji mkuu wa Kampala.

Picha zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha moshi ukifuka katika mji mkuu wa kampala huku vyombo vya habari vikiripoti kwamba maandamano hayo yanafanyika katika mtaa wa mabanda wa kamwokya ambapo mbunge huyo alikulia.

881 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!