Askofu huyo aliyeongoza ibada ya mazishi ya gwiji wa muziki nchini Marekani Aretha Franklin ameomba msamaha baada ya kushutumiwa kwa kumgusa kifua mwanamuziki Ariana Grande mbele ya umati mkubwa uliohudhuria mazishi hayo.

Picha zinamuonyesha Askofu Charles H Ellis wa tatu akimshika Ariana juu ya kiuno chake huku vidole vyake vikiwa vimeshikilia upande mmoja wa kifua chake.

”Sio lengo langu kumshika mwanamke matiti”, aliambia shirika la habari la AP.

”Pengine nilivuka mpaka, pengine nilijihisi kuwa karibu naye sana kama rafiki”.

Aliongezea: lakini tena naomba msamaha. Muhubiri huyo balisema kuwa aliwakumbatia wasanii wote waume kwa wake wakati wa shrehe hiyo ya kumuaga malkia wa muziki wa soul.

Lakini waliohudhuria walianza kutuma picha kutoka katika ibada hiyo wakati Ariana aliposimama na kuanza kuimba wimbo wa Aretha Franklin { You Make Me Feel a natural Woman}

Please follow and like us:
Pin Share