Kocha aliyefukuzwa kazi Peter Bosz (Kushoto), na Kocha Aliyeajiliwa Peter Stöger(Kulia)

Borussia Dortmund leo tarehe 10 Novemba 2017, imetangaza kumfukuza kazi kocha wake,Peter Bosz na kumuajili Peter Stöger.
Peter Bosz amepoteza michezo 12 tangu ajiunge na klabu hiyo na kitu pekee cha kushangaza ni kwamba Dortmund wamemuajili kocha ambaye ametimuliwa na klabu ya inayoshika mkia wa ligi kuu nchini Ujerumani Bundesliga.
Kuchaguliwa kwa Peter Stöger kumezua gumzo kubwa nchini Ujerumani kwani wadau wengi wa soka wanasema Dortmund wamekosea kumsajili Kocha ambaye mwenye historia mbaya kwenye kufundisha timu za Ujerumani.
Peter Stoger amepoteza mechi 8 na kupata sare 3 kabla ya kutimuliwa na klabu ya FC Cologne ambayo inashika mkia kwenye msimamo wa Bundesliga. Ambapo imeelezwa kuwa ndio kocha wa kwanza kuanza vibaya kwenye tangu ligi hiyo ianzishwe.
Na hii inakuwa ni hatua ya kwanza kwenye historia ya Ligi kuu nchini Ujerumani kwa kocha mwenye karba hiyo kuajiliwa na klabu kubwa nchini humo.

By Jamhuri