Sitanii

Rais Magufuli, Dk. Mpango jengeni wafanyabiashara (5)

Katika makala zilizopita nimeshauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuanzisha Kitengo cha Kuanzisha na Kukuza Biashara. Ni wiki ya tano sasa nikiwa naandika makala hii kuunga mkono uamuzi wa Rais John Magufuli na Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango, kupiga marufuku TRA kufunga biashara ya mtu yeyote hapa nchini, isipokuwa kwa wakwepa kodi sugu, ila hiyo nayo ni lazima iwe ...

Read More »

Rais Magufuli, Dk. Mpango jengeni wafanyabiashara (4)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala yangu kwa kushauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuanzisha Kitengo cha Kuanzisha na Kukuza Biashara. Nimepata mrejesho mkubwa. Nimekuta kumbe vijana wengi wanataka kuanzisha biashara lakini hawafahamu ni wapi pa kuanzia. Sitanii, nimepata fursa ya kusoma kitabu cha Mfanyabiashara Reginald Mengi cha ‘I Can, I Must, I Will’. Ni vema nichukue fursa hii kumpongeza mzee Mengi ...

Read More »

Rais Magufuli, Dk. Mpango jengeni wafanyabiashara (3)

Wiki iliyopita katika makala hii nimezungumzia umuhimu wa kuwa na wafanyabiashara. Nimeeleza wafanyabiashara walivyo na fursa ya kutumia miundombinu inayojengwa kama reli kwa kusafirisha mizigo ya biashara, ndege kuwahi vikao na barabara kwa malori kusafirisha mizigo kila siku tofauti na wafanyakazi wanaosafiri mara moja kwa mwaka. Sitanii, katika muda wa miaka 8 niliyokuwa mwekezaji nimebaini mambo kadhaa. Nimebaini kuwa wapo ...

Read More »

Rais Magufuli, Dk. Mpango jengeni wafanyabiashara (2)

Aya mbili za mwisho za makala hii wiki iliyopita zilisomeka hivi: “Makala hii itakuwa ndefu kidogo. Leo nimeanza na utangulizi. Wiki ijayo, nitaeleza umuhimu wa kujenga wafanyabiashara wazawa. China ilifanya uamuzi huo mwaka 1979 kwa maelekezo ya Deng Xiaoping. Marekani walifanya uamuzi sawa na huu (alioufanya Rais John Magufuli) mwaka 1776. Uingereza, Japan, Denmark na nchi zote zilizoendelea, hadi serikali ...

Read More »

Rais Magufuli, Dk. Mpango jengeni wafanyabiashara

Wiki hii naandika makala kwa kusukumwa na kauli za viongozi wakuu wawili wa taifa hili. Hawa si wengine, bali ni Rais John Pombe Magufuli na Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango. Rais Magufuli ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuepuka kufunga biashara, badala yake wapokee kidogo wanachopewa kama kodi kinachobaki wakubaliane utaratibu wa kukilipa. Dk. Mpango yeye amekuja na maagizo ...

Read More »

Padri Kitunda amenigusa, tujenge uzalendo

Najua baadhi ya wasomaji wangu wanapenda kila wakati tuandike siasa, uchumi na mambo mengine ya kijamii. Leo naomba mniruhusu nichepuke kidogo. Kuna kitu kimenigusa katika ibada niliyohudhuria Jumapili iliyopita katika Parokia yetu ya Roho Mtakatifu ya Kitunda. Paroko Msaidizi, Paul Njoka, alitutaka kanisani tufurahie siku ya Uhuru kwa kuimba nyimbo za uzalendo. Sitanii, amefafanua kwa kina umuhimu wa nyimbo hizi ...

Read More »

Magufuli asante kuwatumbua Dk. Tizeba, Mwijage

Nafahamu leo zimepita siku kadhaa tangu Rais John Magufuli afanye uamuzi wa kuwatumbua Waziri mwenye dhamana ya Kilimo, Dk. Charles Tizeba na huyu aliyekuwa na dhamana ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage. Sijaandika lolote kuhusu kutumbuliwa kwao. Wasomaji wangu mmekuwa mkiniuliza, nina kauli gani? Nikawambia subirini. Sitanii, nakiri kwamba sina ugomvi binafsi na Dk. Tizeba au Mwijage, ila katika ...

Read More »

Miundombinu, umeme uko njia sahihi

Leo nimeamua kusitisha makala ya Raila Odinga na urais wa Kenya ili nami kidogo nishiriki kujadili na kuichambua miaka mitatu ya Rais John Magufuli. Tangu Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli iingie madarakani, yametokea mambo mazuri kadhaa. Binafsi nitajikita katika machache, ambayo yote yanaangukia katika ujenzi wa miundombinu. Naanza na umeme. Umeme ndio msingi wa maendeleo kwa ...

Read More »

Raila Odinga anakuwa Rais Kenya (7)

Wiki iliyopita makala hii iliishia katika aya iliyosema: “Mkakati wake [Raila Odinga] kuitisha kura za maoni kubadilisha Katiba nadhani umefikia tamati. Asante rais kwa kutia mkono wako katika uteuzi wa Odinga na kumshawishi akaukubali,” anasema Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro.” Je, unafahamu kuwa kabla ya uteuzi huu Odinga alikataa uteuzi mara kadhaa? Endelea… Odinga aliwahi kuukataa Ubalozi Maalumu wa Umoja ...

Read More »

Raila Odinga anakuwa Rais Kenya (6)

Wiki iliyopita makala hii iliishia kwa kusema wawili hao (Ruto na Waigui) wanahaha kusafisha majina yao, huku Rais Kenyatta akiwa kimya. Jambo jingine linalomtia tumbo joto (Ruto) ni kitendo cha Odinga kujipenyeza kwenye Mkoa wa Bonde la Ufa, ambao ni ngome kubwa ya Ruto anayeungwa mkono na kabila lake la Wakalenjini. Endelea… Odinga kwa sasa amejenga uswahiba na Seneta wa Baringo, ...

Read More »

Raila Odinga anakuwa Rais Kenya (4)

Wiki iliyopita makala hii iliishia katika aya iliyosema; (Raila) Odinga mwenyewe na Najib Balala (Waziri wa sasa wa Utalii), waliwakilisha masilahi ya Mkoa wa Pwani, huku Kalonzo na Charity Ngilu wakiwakilisha masilahi ya Ukambani. (William) Ruto (kabla hawajafarakana), aliyekuwa ameuacha Ukatibu Mkuu wa KANU, aliuwakilisha vema Mkoa wa Bonde la Ufa katika chombo hicho na kuzoa kura nyingi za kabila ...

Read More »

Raila Odinga anakuwa Rais Kenya (3)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala hii kwa aya iliyosema; Pamoja na Rais Kenyatta kushinikizwa amkamate (Raila Odinga) kwa uhaini, alimtafuta kwa faragha na kuunda naye ushirika ambao unaonekana kuileta pamoja Kenya, ilikuwa inaelekea kutumbukia tena katika machafuko.  Maafikiano haya yamezaa ‘utakatifu’ ambao Wakenya wameubatiza jina la kimombo, handshake. Endelea… Kabla sijaendelea na makala hii ya Odinga, msomaji niruhusu angalau kwa aya mbili tu ...

Read More »

Raila Odinga anakuwa Rais Kenya (2)

Wiki iliyopita niliandika sehemu ya kwanza ya makala hii nikieleza dalili ninazoziona kuwa mwanasiasa mkongwe wa Kenya, Raila Amolo Odinga, anakuwa Rais wa Kenya mwaka 2021. Odinga ambaye Wakenya wengi wanamwita “Baba”, amefahamika na kuwa kipenzi cha karibu makabila yote ya Kenya kwa sasa.  Baada ya makala hiyo, nimepokea ujumbe mfupi na simu nyingi kwa kiwango cha kushangaza. Baadhi ya ...

Read More »

Odinga anakuwa Rais Kenya

Balile

Na Deodatus Balile, aliyekuwa Mombasa Kuna kila dalili kuwa mwanasiasa Raila Amolo Odinga (73), miaka minne ijayo atachaguliwa kuwa Rais wa Kenya, yaani mwaka 2021. Hivi karibuni nimepata fursa ya kuwa jijini Nairobi na baadaye nikasafiri hadi Mombasa, ambako nimepata fursa ya kukaa na watu wa kada mbalimbali wanaozifahamu siasa za Kenya. Sitanii, katika nyakati tofauti watu niliozungumza nao hitimisho ...

Read More »

Mfugale Flyover ni ukombozi

Balile

Na Deodatus Balile Kwa muda mrefu ninapokuwa safarini huangalia jambo la kurejea nalo nyumbani. Nimesafiri nchi kadhaa duniani, hivyo nashukuru Mungu kuwa kusafiri huko kumeniongezea uelewa. Katika nchi nyingi, iwe zilizoendelea au zinazoendelea, zimeweka mtazamo na msisitizo mpya katika miundombinu. Nchi nyingi zimebaini kuwa maendeleo ya kweli yanatokana na urahisi wa mawasiliano (Teknohama), miundombinu – barabara, reli, magati ya majini, ...

Read More »

Mfugale Flyover ni ukombozi

Na Deodatus Balile Kwa muda mrefu ninapokuwa safarini huangalia jambo la kurejea nalo nyumbani. Nimesafiri nchi kadhaa duniani, hivyo nashukuru Mungu kuwa kusafiri huko kumeniongezea uelewa. Katika nchi nyingi, iwe zilizoendelea au zinazoendelea, zimeweka mtazamo na msisitizo mpya katika miundombinu. Nchi nyingi zimebaini kuwa maendeleo ya kweli yanatokana na urahisi wa mawasiliano (Teknohama), miundombinu – barabara, reli, magati ya majini, ...

Read More »

MV Nyerere imeamsha uchungu

MV Nyerere imeamsha uchungu Na Deodatus Balile Ajali ya MV Nyerere iliyotokea Septemba 20, 2018 katika Ziwa Victoria imeamsha uchungu wa wakazi wa Kanda ya Ziwa. Imenikumbusha siku ya Jumanne ya Mei 21, mwaka 1996 ilipozama meli ya MV Bukoba na kuua watu zaidi ya 800. Takwimu zinatofautiana. Wapo wanaosema walikufa watu 1,000 na wengine wanasema walikufa 800. Vivyo hivyo ...

Read More »

Lissu ameumizwa, lisitokee tena Tanzania

Na Deodatus Balile Leo nimeona niandike mada inayohusiana na hali ya usalama, amani, utulivu na upendo kwa taifa letu. Nimesoma maandishi ya Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, wakati anatimiza mwaka mmoja wa maumivu tangu alipopigwa risasi Septemba 7, 2017 jijini Dodoma. Si nia yangu kurejea aliyoyasema Lissu, ila kwa picha ya video niliyoiona, inayoonyesha kuwa mfupa wake wa ...

Read More »

Utawala wa sheria utatuepusha ya Makonda

Na Deodatus Balile Wiki tuliyoimaliza imekuwa na matukio mengi. Tumesikia kifo cha Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Mtawa Susan Bathlomeo. Kifo hiki kimeacha maswali mengi. Wapo wanaosema amejirusha, wapo wanaosema amerushwa kutoka ghorofani. Mpaka sasa uchunguzi unaendelea na hatujapata jibu kamili. Sitanii, mwezi Agosti umekuwa na vifo vingi kwa kiwango cha kutisha. Wakati tunaomboleza kifo ...

Read More »

Tamu, chungu ya Magufuli

Na Deodatus Balile Leo zimepita wiki mbili bila kuandika katika safu hii. Makala yangu ya mwisho niliahidi kuandika yaliyojiri katika safari ya mwisho niliyokwenda Mwiruruma, Bunda kumzika Comrade Shadrack Sagati (Mungu ailaze mahala pema peponi roho yake). Sentensi ya mwisho katika makala yangu ilisema: “Olwo mumywanyi wawe kufa afelwa.” Hii ina maana, kuliko rafiki yako kufariki dunia, ni bora afiwe. ...

Read More »

Waziri Lugola maliza sakata la Lugumi

Ni miaka miwili na nusu sasa tangu Watanzania walipoanza kusikia kuhusu sakata la Kampuni ya Lugumi Enterprises kushindwa kufunga vifaa vya kuchukulia alama za vidole kwenye vituo 108 vya Polisi, kama mkataba wa kampuni hiyo na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ulivyotaka. Jambo hilo liliibuliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Juma Assad, ...

Read More »

Rais Magufuli fungua milango zaidi

Na Deodatus Balile   Wiki iliyopita Rais John Pombe Magufuli amefungua milango ya kukutana na viongozi wastaafu. Amekutana nao Ikulu na akasema utaratibu huu ataundeleza. Akasema atakutana nao mara kwa mara na katika kukutana nao hakuwabagua. Amekutana na wale walioko Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hata wale waliohamia upinzani kama Edward Lowassa na Frederick Sumaye. Sitanii safu hii ni fupi. ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons