Habari za Kimataifa

Waziri Mkuu apigwa yai

Waandamanaji wamempiga kwa yai Waziri Mkuu wa Australia, Scott Morrison. Mkasa huo dhidi ya waziri mkuu ulitokea wakati wa mkutano wa kampeni Jumanne wiki iliyopita, bila kusita, walimtandika yai la kichwa. Vipande vya video vya tukio hilo vilionyeshwa kwenye televisheni za nchi hiyo. Walinzi wa waziri mkuu huyo mara baada ya kitendo hicho, haraka sana, wakamdaka mwanamke mmoja miongoni mwa ...

Read More »

Marais wataka uuzaji pembe za tembo

Nchi tano za kusini mwa Afrika zenye idadi kubwa ya tembo zimeanza kudai haki ya kuuza pembe za wanyama hao kwa msisitizo kuwa rasilimali hiyo iwekewe utaratibu utakaonufaisha wakazi wa maeneo ya mapori wanamohifadhiwa. Marais kutoka nchi za Botswana, Zimbabwe, Zambia na Namibia, pamoja na Waziri wa Mazingira kutoka Angola walikutana wiki iliyopita mjini Kasane, Botswana, kuweka sera ya pamoja ...

Read More »

Nigeria kutoa rais wa UNGA

Baada ya miaka 30 kupita Nigeria inaweza kutoa rais wa Baraza la Umoja wa Mataifa (UNGA). Kwa mara ya mwisho Joseph Nanven Garba ndiye aliyekuwa Rais wa UNGA mwaka 1989 kutoka Nigeria. Profesa Tijjani Muhammad Bande ambaye kwa sasa ni mwakilishi wa kudumu wa Nigeria katika Umoja wa Mataifa, ndiye anatarajiwa kushika urais wa UNGA kutoka kwa rais wa sasa, ...

Read More »

Tukio la Papa Francis Vatican latikisa dunia

Baba Mtakatifu, Papa Francis, katika hali isiyotarajiwa amebusu miguu ya Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, akimsihi pamoja na wenzake kuhakikisha nchi hiyo hairudi kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe. Papa Francis amemwomba Rais Kiir na makamu wake wa awali, Riek Machar, ambaye ameasi kwa sasa, pamoja na makamu wengine wa rais waliofika Vatican kuheshimu makubaliano waliyotia saini ya kusitisha ...

Read More »

Waziri Mkuu anena

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema serikali imejiandaa kumjibu Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), kwa ushahidi; na sasa inachofanya ni kumsubiri arejee nchini. Amesema serikali inatambua kuwa Lissu anatibiwa, na kwa maana hiyo si jambo la busara kujibizana na mgonjwa. Waziri Mkuu ametoa msimamo huo katika mahojiano maalumu na JAMHURI yaliyofanyika ofisini kwake jijini Dodoma muda mfupi kabla ya ...

Read More »

Bwawa laua mamia Brazil

Watu 300 wanahofiwa kufariki dunia baada ya bwawa la maji kuvunja kingo zake katika mgodi wa kampuni ya chuma kusini mashariki mwa Brazil. Maji yaliyochanganyika na matope yaliwafunika mamia ya wafanyakazi wa shirika hilo. Shughuli ya kuwatafuta walionusurika inaendelea karibu na mji wa Brumadinho, katika Jimbo la Minas Gerais. Gavana wa jimbo hilo, Romeu Zema, amesema kuna hofu huenda watu ...

Read More »

Mzozo wa kisiasa Venezuela wasambaa kimataifa

Baada ya maandamano ya kumshinikiza Rais Nicolas Maduro kung’atuka madarakani kukumbwa na vurugu, kiongozi mashuhuri wa upinzani, Juan Guaido, amejitangaza kuwa rais wa mpito. Guaido amepata uungwaji mkono kutoka mataifa ya Marekani, Canada na majirani wa taifa hilo walio na ushawishi mkubwa katika Kanda ya Amerika Kusini kama vile Brazil, Colombia na Argentina. Muungano wa Ulaya umetoa wito wa kufanywa ...

Read More »

Congo yawapuuza wanaobeza uchaguzi

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekataa katakata wito uliotolewa na Umoja wa Afrika (AU) kucheleweshwa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais. AU wanasema kuwa wana wasiwasi mkubwa kuhusu uadilifu wa matokeo ya mapema ambayo yalimpatia ushindi, Felix Tshisekedi. Kiongozoi mwingine wa upinzani, Martin Fayulu, ameitaka mahakama ya kikatiba kufutilia mbali matokeo hayo akidai kwamba ndiye mshindi wa ...

Read More »

Watu 70 waungua moto

Mexico Bomba la mafuta nchini Mexico limelipuka na kuua watu zaidi ya 70 huku wengine 71 wakijeruhiwa vibaya baada ya watu wasiofahamika kutoboa bomba hilo kwa nia ya kuiba mafuta. Katika mji wa Tlahuelilpan, Jimbo la Hidalgo, mwishoni mwa wiki ulikuwa katika kilio kikubwa kutokana na mlipuko huo. Taarifa zinasema mamia ya watu walikuwa waking’angania kuchota mafuta kabla ya moto ...

Read More »

Mwandishi auawa ubalozini

Mwanahabari, Jamal Khashoggi, aliuawa katika vita katika Ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul, runinga ya taifa hilo imesema ikinukuu uchunguzi wa awali. Naibu Ofisa Mkuu wa Idara ya Ujasusi, Ahmad al-Assiri na Mshauri Mkuu wa Mwanamfalme Mohammed Bin Salma Saud al-Qahtani walifutwa kazi kufuatia kisa hicho. Wakati huohuo, Uturuki imeapa kufichua maelezo yote kuhusu mauaji ya mwandishi huyo baada ya ...

Read More »

Canada yarasmisha bangi, waishiwa

Wiki iliyopita imekuwa ya kihistoria nchini Canada, kwani serikali ya nchi hiyo baada ya kufanya utafiti kwa muda mrefu hatimaye imefikia uamuzi wa kuruhusu matumizi binafsi ya bangi kwa watu wake. Maduka yalianza kuuza bangi saa 06:01 usiku wa kuamkia Jumatano wiki iliyopita, baada ya awali serikali ya nchi hiyo kuwa imetumia miaka miwili kutunga sheria za kurasmisha matumizi ya ...

Read More »

Matajiri Afrika wanavyotekwa

Tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji, maarufu kama Mo, limeitikisa Tanzania, lakini si jipya kwa mwaka huu barani Afrika. Mo ni tajiri mkubwa wa saba barani Afrika kutekwa tangu mwaka 2018 ulipoanza. Matukio mengine ya namna hiyo yametokea nchini Afrika Kusini, Msumbiji na Nigeria. 1. Shiraz Gathoo – Afrika Kusini Mfanyabiashara maarufu kutoka Afrika Kusini alitekwa Machi 10, mwaka ...

Read More »

Kanye West adai kofia ya Trump imempa nguvu za Superman, akosoa shule za siku hizi

Si jambo la kushangaza kusikia Kanye West mmoja kati ya wasanii maarufu zaidi duniani katika miondoko ya kufoka foka amekutana na Rais wa Marekani Donald Trump. Kwa muda mrefu sasa amekuwa akionyesha hisia zake wazi wazi za kumsifu Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter na mahojiano mbali mbali. Hata hivyo amekuwa akiwakosoa wanaomkemea kwa kuwataka wamwache awe na uhuru wa ...

Read More »

MULTICHOICE YAZINDUA RASMI KITUO CHA MAFUNZO YA UANDAAJI FILAMU AFRIKA MASHARIKI

MultiChoice Africa imezindua rasmi kituo cha mafunzo ya uandaaji wa filamu  katika ukanda wa Afrika Mashariki . Sherehe za uzinduzi huo zimefanyika mjini Nairobi nchini Kenya katika makao makuu ya ofisi ya MultiChoice na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya filamu pamoja na wawakilishi mbalimbali wa serikali  kutoka katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki. Baadhi ya viongozi wa ...

Read More »

Watu 50 wakiwemo watoto 7 wapoteza maisha Kenya

Watu wasio pungua 50 wameuwawa baada ya basi kuacha njia na kupinduka katika mteremko mkali na kugonga magharibi mwa Kenya, afisa mmoja wa usalama amesema Jumatano. Ajali hiyo imetokea saa kumi alfajiri na katika ya wale waliopoteza maisha saba ni watoto, ameongeza. Paa la basi hilo lilifumuka wakati wa ajali hiyo. Kiasi cha manusura 15 kutoka katika basi hilo ambalo ...

Read More »

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley ajiuzulu

Balozi wa marekani kwenye Umoja wa mataifa Nikki Haley ametangaza kujiuzulu. “Imekuwa ni heshima ya maisha” alisema Nikki Hailey akiwa na Rais Donald Trump huko White house alipotangaza kujiuzulu nafasi yake huku akiongeza kwamba haondoki mpaka mwisho wa mwaka. “Tutakukumbuka sana Trump alimwambia Hailey “umefanya kazi nzuri sana”. Akimshukuru Haley kwa kazi yake, Trump alimwelezea mwanadiplomasia huyo kama mtu muhimu ...

Read More »

Uingereza imeitaka Saudia kutoa maelezo ya kina juu ya kupotea kwa Mwandishi

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza amesema kuwa taifa lake linatarajia majibu ya msingi kutokana na kupotea kwa mwandishi wa Saudia Jamal Khashoggi ambaye mara ya mwisho alikuwa katika ubalozi wa Saudi nchini Uturuk Katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Waziri wa mambo ya nje wa Saudia Adel al-Jubeir,Jeremy Hunt amesisitiza kuwa urafiki unapaswa kuzingatia uzingatiaji wa ...

Read More »

Kimbunga Michael kuyakumba majimbo matatu Marekani

Takriban watu nusu milioni wanatakiwa kuondoka haraka katika makazi yao eneo la kusini mashariki mwa Marekani ili kukupisha kimbunga Michael ambacho kinakaribia kulikumba eneo hilo. Taarifa za watabiri wa hali ya hewa zinasema kimbuka hicho kwa sasa kimekwisha ingia katika hatua ya tatu na kuongezeka kasi yake kwa kadri kinavyopitia ghuba ya Mexico kuelekea Jimbo la Florida,Alabama na Georgia. Kimbunga ...

Read More »

Rais Korea Kusini afungwa kwa rushwa

Seoul, Korea Kusini Rais mstaafu wa Korea Kusini, Lee Myung-bak, amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela pamoja na faini ya dola za Marekani milioni 11.5 (sawa na zaidi ya Sh bilioni 25) kutokana na kukutwa na hatia ya makosa kadhaa ya rushwa. Rais Lee alihukumiwa katika Mahakama ya Seoul wiki iliyopita kwa tuhuma za rushwa, ubadhirifu na matumizi mabaya ya ...

Read More »

Rais Recep Tayyip Erdogan aihoji Saudia kutoweka kwa Mwandishi

Rais wa Uturuk Recep Tayyip Erdogan ameitaka Saudia kutoa ushahidi kuhusiana na mwandishi wa habari aliyepotea kwamba alitoka nje ya majengo ya ubalozi wao mjini Istanbul. Mwandishi huyo raia wa Saudia Jamal Khashoggi kwa mara ya mwisho alionekana katika jengo hilo la ubalozi wiki iliyopita.Hapo jana Rais Trump alielezea kusikitishwa kwake kutokana na kutoweka kwa mwandishi huyo. Uturuki imeomba kufanya ...

Read More »

Rais Donald Trump Amwagia Sifa Jaji mkuu mteule

Rais wa Marekani Donald amemuomba radhi kwa niaba ya raia wa Marekani Jaji mkuu mpya Brett Kavanaugh kwa kile alichokiita kwamba ni kampeni chafu za kisiasa zilizolenga kuharibu sifa binafsi ya Brett kutokana na mambo ya uzushi na uongo. Trump ameyasema hayo katika sherehe za kuapishwa kwa jaji huyo mkuu wa mahakama ya juu ya Marekani shughuli ambazo zimefanyika katika ...

Read More »

MWANZA NA MWANDISHI WETU   Wanafunzi 12 wa Sekondari ya Igokelo, Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, wamegundulika kuwa na ujauzito mwaka huu, hivyo kulazimika kuwa kando na masomo yao. Mimba hizo zimewalenga zaidi wanaosoma kidato cha kwanza, cha pili, tatu na nne walio na umri chini ya miaka 18. Mbali na na hayo, imegundulika pia baadhi ya wanafunzi wengine wa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons