MCHANGANYIKO

Yah: Ningependa Rais ajaye afanye yafuatayo?

Wiki jana niliandika barua kama hii nikisema huyu ndiye mwenye sifa za kuwa Rais wa awamu ya tano, niliainisha sifa chache kutokana na ujinga wangu, sifa ambazo baadhi ya watu wanaweza kusema kwa utaratibu wa maisha ya sasa ya utandawazi siyo rahisi kumpata kiongozi mwenye sifa hizo.

Read More »

Ujana, uzee sio sifa za kuwa Rais wa Tanzania

Ni Kitambo sasa, Watanzania wamo katika fikra na harakati za kumpata Rais mpya hapo mwakani, kwa kipindi cha miaka mitano ijayo baada ya Rais wa sasa Profesa Jakaya Mrisho Kikwete kukamilisha muda wake wa uongozi na utawala wa miaka kumi.

Read More »

Huduma mbovu za jamii zitaangusha CCM

Tunapozungumzia huduma za jamii huwa tunazungumzia masuala ya elimu, afya ,maji, umeme, huduma kwa wazee, huduma kwa walemavu na kadhalika.

Read More »

Majibu kwa porojo za Nyalandu

Asoma na kujibu kiubabaishaji tuhuma kwenye magazeti aliyodai awali kuwa ni ya kufungia maandazi. Kwa muda mrefu sasa baadhi ya magazeti hapa nchini yamekuwa yakiujuza umma ukweli kuhusu Lazaro Nyalandu, ambaye kwa takriban miezi tisa sasa ni Waziri wa Maliasili na Utalii. Habari kumhusu Nyalandu zilianza kutolewa hata kabla hajawa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, wakati angali Naibu Waziri katika Wizara ya Viwanda na Biashara, chini ya Cyril Chami wakati huo. Katibu Mkuu wa Wizara hiyo wakati huo alikuwa Joyce Mapunjo.

Read More »

Balozi Mushi nakuunga mkono, ushoga hapana

Mpendwa msomaji natumaini hujambo kiasi. Nakushukuru wewe na wengine kwa ujumbe na mrejesho mkubwa mlionifikishia wiki iliyopita, baada ya makala yangu ya kuomba Watanzania tusifanye majaribio katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Read More »

Mwekezaji alivyomvuruga Kamishna Madini

Mwekezaji katika migodi ya madini ya ujenzi, Majaliwa Maziku, anadaiwa kumlaghai Kamishna wa Madini nchini Tanzania, Paul Masanja, ili kufanikisha azma yake ya kupora ardhi ya wananchi kinyume cha sheria ya madini.

Read More »

Kunani tena kwa Hasheem Thabeet?

Klabu ya Pistons inayoshiriki kwenye Ligi ya Kikapu ya Marekani maarufu kama NBA, imemtema rasmi mchezaji Mtanzania, Hasheem Thabeet, pamoja na nyota wengine wanne.

Read More »

Rage azitabiria mabaya Simba, Yanga

Mwenyekiti mstaafu wa Simba ya jijini Dar es Salaam, Ismail Aden Rage, amesema kwamba michuano ya Ligi Kuu Bara msimu huu itakuwa ngumu kwa timu za Simba na Yanga.

Read More »

Ole kwa mabenki!

Miezi kadhaa nyuma nilikuwa safarini katika moja ya miji iliyopo Nyanda za Juu Kusini. Nilipofika stendi kuna kitu kimoja kilinivutia na nikaamua kukitafakari kwa umakini zaidi.

Read More »

Jifunze namna ya kuunda kampuni

Ni ukweli usiofichika kuwa biashara na ujasirimali  kwa pamoja vimekua  kwa kiwango kikubwa. Hili linatokana na sababu nyingi ikiwemo ya kukua kwa biashara za kimataifa, maendeleo ya mawasiliano, marekebisho ya baadhi ya sera za nchi na sababu nyingine kadha wa kadha.

Read More »

Yah: Kipi kiwe kigezo cha urais kwa sasa Tanzania?

Mwaka 1995, Mwalimu Nyerere alisimama katika majukwaa ya kuongea na wananchi juu ya kiongozi safi na anayefaa kuiongoza nchi yetu katika awamu ya tatu, alisimama akaongea mengi sana ambayo mengine hadi leo hayajafanyiwa kazi na awamu zote zilizokuwapo na kupita.

Read More »

Miaka 69 ya Umoja wa Mataifa, dunia iko salama?

Ijumaa iliyopita Oktoba 24, mwaka huu ulimwengu uliadhimisha miaka 69 tangu kuanzishwa Jumuiya ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York nchini Marekani. Ilikuwa ni baada ya Vita Kuu vya Pili ya Dunia kumalizika (1939-1945).

Read More »

Ombwe kamwe halikubaliki

Mwenyezi Mungu alipoumba dunia yetu alipanga kila kitu kujiendesha kwa namna ya ajabu. Viumbehai na visivyokuwa hai vyote vilipangiliwa kimaajabu kabisa kwa kadiri ya huo utaratibu wa Muumba wetu. 

Read More »

Athari za Serikali kupuuza vyombo vya habari

Sisi sote tunatarajia vyombo vya  habari na mchango wake wa Taifa letu. Kwa jumla vyombo vya habari hufanya kazi  tatu. Huelimisha, huchochea maendeleo na huburudisha. Lakini pia vyombo vya habari hupunguza tatizo la ajira. Hutoa ajira.

Read More »

Ujangili Ruaha umepungua, haujakwisha

Alhamisi Oktoba 16, mwaka huu napigiwa simu na Ofisa Habari wa Umoja wa Mataifa (UN), Stella Vuzo, kuwa nimeteuliwa kwenda kuripoti kazi zinazofanywa na Umoja huo katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Read More »

Uwezo wa kumpiga tunao, Sababu ya kumpiga tunayo

Hotuba ya Mwalimu Julius Nyerere aliyoitoa tarehe 2 Novemba, 1978 alipokuwa akitangaza vita vya kupambana na uvamizi wa majeshi ya Idd Amini katika ukumbi wa Diamond Jubilee

Read More »

Sumaye awe mkweli, hajawahi kuichukia rushwa

Nianze kwa maneno mepesi. Anachokifanya sasa hivi Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, ni kutapatapa. Amegeuka kuwa mtu wa kulalama na kulalamika kila uchao utadhani ndiyo kwanza “anazaliwa”, na wala hajawahi kuwa mmoja wa  vigogo wakubwa kabisa Tanzania.

Read More »

Tusifanye majaribio katika urais 2015

Kadri muda unavyozidi kusonga mbele naona joto la kuwania urais linapanda. Joto hili linapanda kwa wanasiasa, wapambe wao na hata viongozi walioko madarakani wanaanza kuangaliangalia nani watamsaidia kushika dola kisha aendelee ‘kuwaenzi’.

Read More »

Hivi kweli Kaburu ni kirusi Simba, soka la Tanzania?

KWENYE wallet (pochi ya kutunzia fedha) ya kada wa klabu ya Yanga, Sudi ‘Tall’ Hussein pamoja na kuchukua mambo mengine ndani yake kuna kipande cha gazeti la michezo la MWANAspoti.

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons