Habari za Kitaifa

Yaliyowakuta wanahabari gerezani

Hatimaye waandishi wa habari, Christopher Gamaina na wenzake wawili wa jijini Mwanza wameachiwa huru kwa dhamana ya mahakama. Wanakabiliwa na tuhuma ya unyang’anyi wa kutumia nguvu wa Sh milioni tatu, katika kesi namba 11 ya mwaka 2018. Kila mmoja amedhaminiwa na watu wawili kwa kusaini hundi ya maneno ya shilingi milioni tatu, kila mmoja. Kesi hiyo inatokana na kinachodaiwa kuwa ...

Read More »

JWTZ waombwa DRC

Wananchi wa Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wameandamana wakitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lipelekwe nchini humo liwakung’ute waasi wanaoua mamia kwa maelfu ya watu. Bado wananchi wengi wa DRC wanatambua na kuenzi kazi kubwa iliyofanywa na majeshi ya Umoja wa mataifa ya kulinda amani yaliyoongozwa na JWTZ baada ya kuwafurusha waasi wa March 23 ...

Read More »

Wameitelekeza Clock Tower Dar?

Mpita Njia, maarufu kama MN, ameendelea kufurahishwa na pilikapilika za mapokezi ya wageni wa nchi mbalimbali wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). MN ameshuhudia pilikapilika za usafi katika maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam na kipande cha Barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Clock Tower ama Mnara wa Saa uliopo eneo la ...

Read More »

Ngorongoro wapinduana

Uongozi wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro mkoani Arusha umepinduliwa. Waliochukua hatua hiyo wanawatuhumu viongozi hao kwa ufisadi na matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za baraza hilo. Uongozi wote wa juu umeondolewa. Walioondolewa ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji, Edward Maura; Makamu Mwenyekiti wa Baraza, Shutuk Kitamwas na Katibu wa Baraza la Wafugaji, Johanes Tiamasi. Taarifa ya waendesha mapinduzi hao ...

Read More »

Ripoti yafichua madudu uuzwaji shamba la KNCU

Uuzwaji wa shamba kubwa la kahawa la Gararagua lililopo Wilaya ya Siha mali ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro (KNCU) umedaiwa kugubikwa na madudu mengi, ikiwamo kuuzwa chini ya thamani halisi ya bei ya soko, pamoja na kutokujulikana zilipo ekari 2,000. Shamba hilo liliuzwa mwaka 2017 na KNCU kwa dola za Marekanai milioni 4.2 sawa na Sh bilioni 9.24, ...

Read More »

Mtikisiko ajali ya lori Moro

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ameunda timu maalumu kuchunguza tukio la mlipuko wa lori la mafuta ulioua watu 71  na majeruhi 59 kwa mujibu wa takwimu za hadi Jumapili alasiri. Timu hiyo inatarajiwa kukamilisha kazi zake Ijumaa wiki hii na kwa mujibu wa maelezo ya waziri mkuu, ibainishe yeyote ambaye amezembea katika kutimiza wajibu wake kwa wakati kuhusu ajali hiyo ya ...

Read More »

Wakulima Kilombero wanufaika na kilimo endelevu

Mfuko wa Wanyamapori Africa (AWF) umesaidia wakulima wa mpunga na kokoa Kilombero kupitia Mradi wa Ukuaji wa Kilimo Shirikishi na Endelevu Kilombero katika kutoa elimu ya mnyororo wa thamani ili kuwa na kilimo chenye tija. Katika mradi huo wa miaka mitatu ulioanza mwaka 2017, AWF pamoja na wadau wengine imewezesha wakulima zaidi ya 500 katika kupata mbegu bora za kokoa ...

Read More »

Waomboleza

Familia ya Naomi Marijani (36), imefanya maombolezo kwa ibada maalumu baada ya kuthibitika kuwa binti yao ameuawa. Ingawa haijathibitika nani kamuua (kwani kesi ndiyo imeanza), pamoja na mume wake kukiri mbele ya polisi kuwa alimuua na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa nyumbani kwake Gezaulole, Kigamboni, Dar es Salaam na kisha kuzika mabaki shambani kwake Kijiji cha Marogoro, ...

Read More »

Mfumo wa Tehama kuzilinda barabara

Bodi ya Mfuko wa Barabara imo mbioni kuzindua mfumo wa Teknolojia na Mawasiliano (Tehama) utakaowashirikisha wananchi katika kufuatilia uharibifu na matengenezo ya barabara. Lengo la kuanzishwa kwa mfumo huo ni kuwawezesha na kuwashirikisha watumiaji wa barabara kutoa taarifa kwa mamlaka husika juu ya uharibifu wa miundombinu hiyo. Hayo yamesemwa na Eliud Nyauhenga, Meneja wa Mfuko wa Barabara wakati wa kilele ...

Read More »

Simu ‘yamuua’ Naomi

Siku chache baada ya polisi kutangaza kumkamata Hamis Said Luwongo (38), kwa tuhuma za kumuua na kumchoma moto mke wake, Naomi Marijani, taarifa za kina zimeanza kuvuja na inaonekana simu ya mkononi ilichangia kutokea kwa mauaji hayo. Uchunguzi unaonyesha kuwa miaka mitatu iliyopita, familia ya Hamis na Naomi, iliingia katika majaribu ya hali ya juu baada ya wanandoa hao kutiliana ...

Read More »

Machungu mgogoro wa ardhi Kwimba

Mgogoro wa ardhi uliodumu miaka mitatu sasa baina ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mahiga na familia ya Dionis Mashiba, Wilaya ya Kwimba, Mkoa wa Mwanza, unaonekana kupuuzwa na mamlaka wilayani hapa. Mtanziko huo ulioanza mwaka 2016, unatokana na kile kinachodaiwa kuwa familia ya Mashiba kuingia kwenye eneo la Mwalimu Majenga huku Idara ya Ardhi ikishutumiwa kushindwa kuutatua. Kutokana ...

Read More »

Alivyouawa

Siku chache baada ya Polisi kuthibitisha kwamba Naomi Marijani ameuawa, uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI umebaini kwamba maandalizi ya mauaji yake yalifanyika wiki moja kabla, huku akiishi na mtuhumiwa wa mauaji katika nyumba moja. Uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI umebaini kwamba kulikuwepo na misuguano baina ya Saidi (Meshack) Hamis Luwongo na mkewe, marehemu Naomi Marijani. JAMHURI limethibitishiwa pasi na shaka ...

Read More »

Gamboshi: Mwisho wa dunia (7)

Wiki iliyopita katika sehemu ya 6 hadithi hii iliishia katika aya inayosema: “Sina kitu nitakachopoteza lile dubwasha likinishinda mama yangu. Sana sana nitapoteza roho yangu tu. Sasa roho yangu ikipotea kutakuwa na hasara gani? Je, ni nani ajuaye kwa dhati roho huenda wapi baada ya kifo? “Aliyeiweka roho ndani yangu atajua pa kuipeleka.” Kijana wangu huyu alikuwa anasema kila mara. ...

Read More »

Ameuawa?

Naomi Marijani (36), mama wa mtoto mmoja, mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam ametoweka katika mazingira yenye utata kiasi cha kujengeka hisia kuwa ameuawa, JAMHURI linaripoti. Hadi leo zimetimia siku 63 tangu Naomi ametoweka katika mazingira yenye kuacha maswali mengi huku polisi wa Kigamboni wakionekana kutolipa kipaumbele suala la kupotea kwake, japo ushahidi wa mazingira unabainisha wazi mtuhumiwa wa ...

Read More »

Nchi yapiga hatua zaidi sekta ya afya

Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa kuwa na mashine bora 24 zinazopima makundi ya damu. Mitambo hiyo ya kisasa zaidi ulimwenguni inahusika pia kupima maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwamo homa ya ini na virusi vya ukimwi. Afrika Kusini ndilo taifa la kwanza Afrika kuwa na mashine hizo bora. Aidha, imethibitishwa kuwa, Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika kwa kuwa ...

Read More »

Jinamizi wizi wa magari laibuka

Utata umegubika kuhusu umiliki wa gari la mfanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Moshi, Haika Mawala, lenye namba za usajili T 991 DMS aina ya Toyota Vangurd, baada ya taarifa mpya kuibuka zikidai gari hilo ni la wizi na liliingizwa nchini kwa njia za panya. Gari hilo ni miongoni mwa magari matatu yaliyokamatwa na polisi mkoani Kilimanjaro Septemba 14, ...

Read More »

Waliomdanganya JPM kibao chageuka rasmi

Miezi miwili tangu aliyestahili tuzo ya mfanyakazi bora wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), James Kunena, kupokwa fursa hiyo saa chache kabla ya kutunukiwa na Rais Dk. John Magufuli katika kilele cha mwaka huu cha Mei Mosi, hali si shwari ndani ya Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU). Uchunguzi wa JAMHURI umebaini hali ya ‘hasira’ miongoni mwa wafanyakazi wa ...

Read More »

Vigogo KCBL watelekeza mali za mabilioni

Wafanyakazi wawili miongoni mwa watano waliofukuzwa kazi na Bodi ya Uongozi ya Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) wametoweka na kutelekeza mali za mabilioni ya fedha. Mali hizo ni pamoja na nyumba za kifahari, magari pamoja na viwanja. Ni mali ambazo kwa sasa zipo chini ya ulinzi wa vyombo vya dola kwa ajili ya uchunguzi. Wafanyakazi hao ni aliyekuwa Meneja Mkuu ...

Read More »

‘Wenye ualbino wako salama nchini’

Tanzania imetajwa kufanya vizuri katika kukomesha mauaji dhidi ya watu wenye ualbino. Mwaka 2006 Tanzania iliingia kwenye historia mbaya baada ya watu hao kuanza kuuawa kwa imani za kishirikina. Takwimu zilizotolewa Septemba 21, 2014 na Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) zilibainisha kuwa mwaka 2006 hadi 2014, watu 74 walipoteza maisha kwa mikasa hiyo. Kwa mujibu wa takwimu hizo, ...

Read More »

Serikali, kampuni za simu kusaidia watoto, wanawake

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na kampuni za simu ili kuwasaidia wananchi katika huduma mbalimbali za kijamii zikiwamo za afya, elimu na miundombinu. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Vodacom Tanzania Foundation hivi karibuni, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Joseph Kandege, amesema serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ili kuwawezesha Vodacom kuwafikia Watanzania wote wenye mahitaji.  Waziri Kandege amesema ...

Read More »

Bomu la ardhi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amepata jaribio kubwa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. “Siku moja baada ya kuingia ofisini, alijifungia ofisini kwake akasema ana shughuli nyingi hivyo asingeweza kumwona mtu yeyote. Ghafla, akaja mzee mmoja. Akamweleza msaidizi wake tukio la kusikitisha. Tukio lenyewe lilikuwa kama sinema vile. ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons