Michezo

Watanzania wapewa somo

Wadau mbalimbali nchini wametoa maoni yao mara baada ya wiki iliyopita Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kumtangaza Ettiene Ndayiragije kuwa kocha mkuu wa muda wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars. Kocha huyo anachukua mikoba iliyoachwa na raia wa Nigeria, Emmanuel Amunike, ambaye mkataba wake wa kuifundisha timu hiyo ulisitishwa baada ya Stars kutofanya vizuri katika mashindano ...

Read More »

Lampard kuanza kipimo na vigogo

Wiki iliyopita mchezaji wa zamani wa timu ya Chelsea na West Ham United, Frank Lampard, alitangazwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa Chelsea (The Blues). Timu hiyo inayopatikana katika Jiji la London, Uingereza, imeingia mkataba wa miaka mitatu na Lampard ambaye kabla ya mkataba wake huo wa kuinoa Chelsea alikuwa kocha wa Derby Country, klabu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza England. Lampard ...

Read More »

AFCON acha tu

Wakati michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ikiendelea nchini Misri hii leo ili kukamilisha hatua ya makundi, makundi mawili yataingia uwanjani kupepetana ili kuungana na timu nyingine waweze kufuzu hatua inayofuata ya mashindano hayo. Makundi hayo yaliyosalia ni kundi E na kundi F. Kundi E lina timu za Mali, Angola, Tunisia na Mauritania. Mali yenye pointi nne ambao ...

Read More »

Viungo Stars mhh…

Taifa Stars imeanza vibaya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa kukubali kipigo cha magoli 2-0 dhidi ya Senegal (Simba wa Teranga) katika dimba la Juni 30, jijini Cairo, Misri. Goli la kwanza la Senegal lilifungwa na Keita Balde katika dakika ya 28 ya kipindi cha kwanza. Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha pili baada ya Diatta kufunga ...

Read More »

Mitanange ya kibabe AFCON

Takriban siku tatu zimebaki kabla ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kuanza rasmi mwaka huu. Katika michuano hiyo mechi nyingi zitachezwa katika makundi manne, na kila kundi hujumuisha timu nne. Kuanzia kundi A, ambalo linaongozwa na timu mwenyeji, timu ya taifa ya Misri hadi kundi F. Waandaaji wa mashindano hayo, Misri wakiwa katika kundi hilo la A, wataongozwa ...

Read More »

Kagera Sugar, Mwadui kicheko

Pengine mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba, wangetamani kuona Kagera Sugar hairudi ligi kuu, lakini ndiyo kama ulivyosikia wamerudi. Uzoefu na mipango vimezifanya timu za Kagera Sugar na Mwadui kurejea ligi kuu msimu ujao wa 2019/2020, timu hizo zimefanikiwa kubaki ligi kuu baada ya mechi za marudiano ya ligi ya mchujo. Kagera Sugar imewafunga Pamba ya Mwanza 2-0, katika mchezo ...

Read More »

Stars chunga hawa!

Ligi mbalimbali duniani zimemalizika katika msimu wa 2018/2019. Fainali ya Europa na UEFA nazo zimemalizika, hicho kikiwa ni kiashiria kwamba wachezaji wanakwenda katika mapumziko na kuanza maandalizi ya msimu mwingine wa ligi. Pazia la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya limefungwa Jumamosi iliyopita kwa fainali baina ya Tottenham na Liverpool. Mchezo huo ulipigwa katika dimba la Wanda Metropolitano (uwanja wa Atletico Madrid), ...

Read More »

TFF wanaiachaje Azam TV, RTD?

Ligi Kuu imekwisha kufikia tamati na Klabu ya Simba kutwaa ubingwa. Nitoe pongezi kwa Simba na uongozi wao kwa hatua hiyo kubwa. Lakini mbali na Simba, timu nyingine kadhaa zimeshiriki ligi hiyo kwa mafanikio hata kama si ya kiwango cha kutwaa ubingwa. Katika miaka isiyopungua 10 lilikuwa jambo gumu Watanzania kushuhudia ligi yao ikirushwa moja kwa moja kupitia kituo chochote ...

Read More »

Ligi Kuu hekaheka

Hadi hivi sasa tunaweza kusema timu ya Simba SC, Yanga SC, Azam, KMC, Lipuli na timu ya  Mtibwa Sugar zimefanikiwa kujitengenezea ‘dunia’ ya peke yao katika Ligi Kuu Tanzania Bara, licha ya ligi hiyo kubakiza mechi chache kabla ya kufikia tamati. Hali hiyo inatokana na timu kadhaa zinazoshiriki ligi hiyo kutokuwa na uhakika wa kusalia katika ligi hiyo kuu katika ...

Read More »

Wapinzani wa Messi dhidi ya Simba SC

Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa imezidi kuinogesha Tanzania katika ulimwengu wa soka kiasi cha kuongeza ushindani miongoni mwa timu kubwa hapa nchini. Hii ni kampuni ya michezo ya kubahatisha ambayo imepata kutoa udhamini kwa timu kadhaa hapa nchini, ambazo ni pamoja na Yanga, Simba, Mbao na Singida United. Safari hii, miongoni mwa timu hizo kubwa zilizopata kuwa chini ...

Read More »

Hapatoshi Wydad vs Esperance

Hatimaye timu ya Esperance de Tunis ya Tunisia na Wydad Casablanca ya Morocco zimefanikiwa kufuzu katika hatua ya fainali ya Klabu Bingwa barani Afrika (CAF Champions League). Esperance wameingia fainali baada ya kuwafunga TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo goli 1-0 katika mechi ya raundi ya kwanza wakiwa uwanja wa nyumbani. Katika mchezo wa raundi ya pili wakiwa ...

Read More »

Rekodi za kutisha UEFA

Leo ni leo katika historia ya mashindano ya Klabu Bingwa barani Ulaya (UEFA Champions League), ambapo hakuna historia isipokuwa rekodi maridhawa, wakati Tottenham Hotspurs ya Uingereza ikipambana na Ajax ya Uholanzi, huku kesho mabingwa wenye historia zinazofanana wakimenyama katika dimba la Camp Nou. Ajax imechukua taji hilo mara tatu mfululizo (back to back) kuanzia mwaka 1971 hadi 1973. Imechukua taji ...

Read More »

Bodi ya Ligi gumzo

Hali ya soka nchini hususan mwenendo wa michezo ya ligi kuu si ya kuridhisha. Kumekuwa na lawama kutoka kwa wadau wa soka zinazoelekezwa kwa waamuzi wa mechi mbalimbali, lakini kwa upande mwingine, vilevile kumekuwa na malalamiko dhidi ya Bodi ya Ligi Tanzania Bara. Wakati waamuzi wakilalamikiwa  kutokuwa imara na makini katika baadhi ya mechi wanazosimamia, Bodi ya Ligi imekuwa ikishutumiwa ...

Read More »

Serengeti Boys, tunawategemea

Haikuwa kazi rahisi kwa Serengeti Boys kutawala mchezo kwa kiwango cha asilimia 58 dhidi ya asilimia 42 ya wapinzani wao, Nigeria, katika mechi ya ufunguzi wa Michuano ya Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Ingawa Serengeti Boys ilinyukwa mabao matano kwa manne katika mchezo huo wa Jumapili iliyopita, Kocha wa timu hiyo ...

Read More »

Tambo zaanza kuelekea Afcon

Kocha wa timu ya soka ya taifa ya Uganda, Sebastien Desabre, amesema timu ya taifa ya soka ya Zimbabwe ina nafasi finyu katika kundi ‘A’ kwenye michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baadaye mwezi Juni, mwaka huu. Uganda itakabiliana na mwenyeji wa michuano hiyo, Misri, DR Congo na Zimbabwe katika kundi ‘A’. Kocha huyo kwa upande ...

Read More »

Simba SC ni ‘half time’

Dakika 90 kati ya 180 za mchezo wa robo fainali ya Kombe la Klabu Bingwa barani Afrika baina ya Simba SC na TP Mazembe zimekamilika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa miamba hao kutoka suluhu. Klabu ya Simba imekuwa ikiheshimika huko nje kwa kutumia vema uwanja wake wa nyumbani, hasa ikikumbukwa kwamba ilipata matokeo chanya dhidi ya ...

Read More »

Yanga kutetema mbele ya Lipuli?

Timu ya Yanga imeendelea kugawa dozi kwenye Kombe la FA, baada ya kufuzu kuingia katika hatua ya nusu fainali, baada ya kuwatupa nje ya michuano hiyo timu ya Alliance kwa jumla ya penalti 4-3 katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza, baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1. Katika hatua hiyo ya robo fainali, mchezo huo wa ...

Read More »

Babu Miura bado anakiwasha

Ng’ombe hazeeki maini, Waswahili ndivyo wanavyosema. Kazuyoshi Miura, ndiye anayetajwa kuwa mchezaji wa soka mwenye umri mkubwa zaidi duniani. Inaelezwa kuwa licha ya kuwa na umri wa miaka 52, bado anasakata kabumbu katika timu ya Yokohama inayoshiriki Ligi Kuu nchini Japan. Miura pia anafahamika kwa jina la ‘King Kazu’, kutokana na kucheza miondoko ya ‘kazu’ pindi anapofunga magoli. Miura ni ...

Read More »

‘Bravo’ Simba SC

Haikuwa rahisi kwa timu ya Simba SC kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika. Ni safari ya milima na mabonde lakini hatimaye Simba wamevuka na kuingia katika hatua ya robo fainali, na haikuwa safari ya usiku mmoja. Kauli mbiu mahususi ya ‘Do or Die’ (kufa au kupona) kama viongozi wa Simba walivyoinadi kwa mashabiki wao ilitimia, ...

Read More »

Hesabu kali zapigwa Kombe la FA

Asikwambie mtu, hakuna timu isiyopenda kuitwa timu ya kimataifa, miaka ya hivi karibuni msemaji wa zamani wa Yanga, Jerry Muro, alikuwa akijigamba kuwa timu hiyo ni ya kimataifa kwa sababu wanapanda ndege na wanashindana na timu za nje ya Tanzania. Bila kukinzana na kauli hii, timu nyingi zimekuwa katika mapambano makali ya kufanya vizuri katika fainali ya Kombe la Shirikisho ...

Read More »

Manchester United kufanya maajabu?

Kipute cha Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) wiki hii kinaendelea na leo kutakuwa na mchezo mmoja, miamba ya Hispania, Real Madrid, ikikaribishwa na timu ya Ajax katika mchezo wa marudio utakaofanyika Uwanja wa Johan Cruijjf nchini Uholanzi. Katika mchezo huo Real Madrid itamkosa beki wake kisiki, Sergio Ramos, baada ya kupata adhabu ya kadi mbili za njano katika mechi iliyopita, ...

Read More »

Simba inakula ‘viporo’

Wiki iliyopita timu ya Simba imeendelea kula viporo vyake vema katika mechi zake baada ya kuilaza timu ya Azam kwa magoli 3-1 katika Uwanja wa Taifa. Simba ilipata magoli hayo kupitia kwa Meddie Kagere aliyefunga magoli mawili huku jingine likifungwa na John Bocco, na lile la kufutia machozi la Azam likifungwa na Frank Domayo, hivyo kujiongezea nafasi ya kutwaa ubingwa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons