Michezo

Kenya kuandaa riadha ya vijana wasiozidi miaka 20 mwaka 2020

Bodi ya shirikisho la riadha duniani , IAAF imeuchagua mji mkuu wa Kenya, Nairobi kuwa mwenyeji wa mashindano ya riadha ya ulimwengu ya vijana wenye chini ya umri wa miaka 20 yatakayoandaliwa mwaka 2020. Uamuzi huo wa kuchagua mji huo kama uwanja wa kuandaliwa kwa shindano hilo la kimataifa ni baada ya bodi hiyo kuyataja mashindano ya riadha ya vijana ...

Read More »

Hatima ya Nigeria Kuvuka Hatua ya Makundi Kujulikana Leo Dhidi ya Iceland

Michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi inaendelea kushika kasi tena ambapo Afrika itakuwa inawakilishwa na Nigeria itakayokuwa kibaruani dhidi ya Iceland. Matumaini pekee ya Nigeria kuendelea kusalia kwenye michuano hiyo yataonekana leo endapo itaibuka na ushindi wa mabao mengi huku ikitegemea matokeo ya mechi zingine zilizosalia. Timu hiyo ilipoteza mechi yake ya kwanza ilipocheza dhidi ya Croatia kwa kufungwa ...

Read More »

Kimahesabu Argentina Ishatoka kwenye Hatua ya Makundi Kombe la Dunia

Kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kimeshindwa kutamba mbele ya Croatia baada ya kukumbana na kichapo cha mabao 3-0. Mabao ya mchezo huo wa kundi D yaliwekwa kimiani na Luca Modric, Ivan Rakitic na Ante Rebic. Kufuatia kichapo hicho walichokipata Argentina kinawafanya wasalie na alama moja waliyoipata dhidi ya Iceland baada ya kwenda sare ya 1-1 wakiwa nafasi ya ...

Read More »

REKODI YA YANGA SC TANGU AONDOKE LWANDAMINA

Hapa nimekuwekea michezo na Matokeo yote waliyoyapa yanga baada ya Kuondoka kocha wao  Lwandamina   Aprili 11, 2018; Yanga 1-1 Singida United (Ligi Kuu Dar es Salaam) Aprili 18, 2018; Welayta Dicha 1-0 Yanga SC (Kombe la Shirikisho) Aprili 22, 2018; Mbeya City 1-1 Yanga SC (Ligi Kuu Mbeya) Aprili 29, 2018; Simba 1 – 0 Yanga SC (Ligi Kuu ...

Read More »

Deogratius Munishi ‘Dida’: Sina Mpango Kurudi Kucheza Soka Bongo

KIPA wa zamani wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kurejea kucheza tena nchini katika timu yoyote ya Ligi Kuu Bara ikiwemo Yanga kwa kuwa anataka kufika mbali zaidi katika upande wa soka la kulipwa. Dida ambaye anacheza katika Klabu ya Chuo Kikuu cha Pretoria ‘Tucks FC’ inayo­shiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Afrika Kusini, amekuwa ...

Read More »

Yanga Yapania Kushinda Mechi zote Zilizobakia

Baada ya kusalimu amri kwa kuipa nafasi Simba ya kuutwaa ubingwa wa ligi msimu huu, Yanga wamesema watapambana kushinda mechi zote zilizosalia. Kupitia kwa Afisa wa Habari wa Yanga, Dismas Ten, ameeleza kuwa Yanga inahitaji heshima ya kushinda mechi zote zilizosalia ili kulinda heshima yao. Ten anaamini ushindi wa mechi zilizosalia utathibitisha kuwa wao ndiyo mabingwa wa taji la ligi ...

Read More »

SIMBA SC KAZINI LEO KUUMANA LIPULI FC

Kikosi cha Simba kinashuka dimbani Uwanja wa Samora mjini Iringa kikiwa mgeni dhidi ya Lipuli. Simba itakuwa inacheza bila kiungo wake Jonas Mkude ambaye atakosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano. Mkude atalazimika kusubiri mechi dhidi ya watani zake wa jadi utakaopigwa Aprili 29 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Kiungo James Kotei ndiye atakuwa mbadala wa ...

Read More »

YANGA SC KUWA KWENYE KUNDI GANI? ITAJULIKANA LEO

Droo ya upangaji wa timu zitakazokutana hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika inatarajia kufanyika Jumamosi ya leo Aprili 21 2018. Jumla ya timu 16 zimeshatinga kuingia hatua hiyo baada ya michezo 16 kupigwa ndani ya wiki hii. Yanga kutoka Tanzania ni timu pekee inayotuwakilisha kimataifa nayo imetinga hatua hiyo baada ya kuiondoa Wolaita Dicha SC kutoka Ethiopia kwa ...

Read More »

YANGA WAPO FITI KUWATUPA NJE YA MASHINDANO WAITHIOPIA LEO

Mmoja wa viongozi wa Yanga nchini Ethiopia, Hamad Islam, amesema kwamba; “Wachezaji wanafanya mazoezi mara mbili kwa siku na tuko tayari kwa mchezo. Hali ya hewa ni nzuri siyo baridi kali sana, inafanana na ya Dar ilivyo kwa sasa, mechi ni saa 10 jioni.”   “Tuombeane kwani Yanga imebeba bendera ya nchi kwa sasa, tunataka tuhakikishe tunapata bao, hatujaja hapa ...

Read More »

John Bocco: Lipuli Kaeni Chonjo Jumamosi

John Bocco, amesema Lipuli ijiandae kupokea kipigo kwa kuwa lengo lao kubwa ni kupata ubingwa. Mchezaji huyo ambaye jana alifunga bao la kwanza wakati Simba ikiifungaTanzania Prisons Uwanja wa Taifa, amesema mechi na Lipuli si ya kubeza lakini sisi tupo vizuri. Bocco ameeleza kuwa wanaijua Lipuli vizuri na watacheza kwa kujituma ili kupata matokeo waweze kutenegeza mazingira mazuri ya kuwa ...

Read More »

OKWI AMTIA HOFU AMISI TAMBWE KWA KASI YA UFUNGAJI

Staika mkongwe wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga, Amissi Tambwe ameanza kuingiwa na hofu ya kumuona Emmanuel Okwi wa Simba akivunja rekodi zake katika Ligi Kuu Bara huku akisema jamaa ni balaa. Tambwe, raia wa Burundi, ana rekodi nyingi katika ligi kuu ikiwemo ile ya ufungaji bora mara mbili katika msimu wa 2013/14 akifunga mabao 19 na msimu ...

Read More »

Ruvu Shooting ilistahili kushinda Mechi Yao Dhidi ya Azam FC

Kikosi cha Ruvu Shootinga kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Mabatini, Mlandizi jana. Mchezo umepigwa jana baada ya kuahirishwa juzi Alhamis kufuatia mvua kali kunyesha iliyosababisha maji kujaa Uwanjani. Mabao ya Ruvu yamefungwa na Khamis Mcha katika dakika ya 29 kipindi cha pili huku bao la pili ...

Read More »

Simba Sc Yaendelea Kutunza Rekodi ya Kutokufungwa Ligi Kuu Bara

SIMBA SC imeendelea kushikiria record yake ya kutokufungwa kwenye Ligi Kuu baada ya leo kuifunga Mbeya City kwa Mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ushindi huo unawafanya Simba wafikishe pointi 55 baada ya kucheza mechi 23, moja zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 47 katika nafasi ya pili. Katika mchezo huo uliochezeshwa na Mwamuzi, Hance ...

Read More »

NCAA YADHAMINI NGORONGORO MARATHON

Mashindano ya Ngorongoro Marathon 2017, ambayo kwa mara ya kwanza yalidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Mamlaka hiyo inadhamini kwa mara ya pili mwaka huu. (Picha na Yusuph Mussa).   Na Yusuph Mussa, Tanga MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongo (NCAA) imedhamini mashindano ya Ngorongoro Marathon kama sehemu ya njia ya kukuza utalii kwenye eneo hilo lenye vivutio vya ...

Read More »

Simba Yazidi Kuukaribia Ubingwa, Yaikung’uta Mtibwa Sugar Bao 1-0

Simba SC imeendelea kujikita kileleni katika Ligi Kuu Bara baada ya kuitandika Mtibwa Sugar  bao 1-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Mchezo huo uliokuwa unaambatana na mvua iliyokuwa ikinyesha Uwanjani, ulishuhudiwa nyavu zikitikiswa mnamo dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza na Emmanuel Okwi. Okwi alifunga bao hilo akimalizia kazi mpira wa kichwa kutoka kwa John Bocco na kufanya ...

Read More »

Simba Kazini Leo Dhidi ya Mtibwa Bila Majembe Haya

SIMBA SC itawakosa wachezaji wake watatu, mabeki Mganda Juuko Murshid, mzawa Erasto Nyoni na kiungo Mghana, James Kotei katika mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar leo Jumatatu Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kutokana na kutumikia adhabu ya kadi za njano. Lakini kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa Pierre Lechantre anajivunia kurejea kwa, Jonas ...

Read More »

Rufani ya Michael Richard Wabura Bado Kitendawili

Rufani ya Michael Richard Wambura bado kitendawili na hili ni baada ya kamati ya rufaa kuchelewa kutoa maamuzi. Je ni sahihi maamuzi kuchelewa ili haki itendeke au si sahihi kwa kuwa kamati hii imepokea taarifa ya pande zote mbili? Hebu tuzungumze hapa juu ya kile unachokiona kwenye sakata hili kwa kutoa comment yako.  

Read More »

Liverpool Yaiadhibu Manchester City Kombe la UEFA

Michuano ya UEFA Champions League hatua ya robo fainali usiku wa April 4 2018 iliendelea tena kwa michezo miwili kupigwa, FC Barcelona wakiwa katika uwanja wao wa Nou Camp walicheza dhidi ya AS Roma wakati Liverpool walicheza na Man City katika dimba la Anfield. Game kati ya Liverpool dhidi ya Man City ndio ilikuwa inasubiriwa kwa hamu usiku huo, hii ...

Read More »

Simba Sc Mzigoni Leo Kusaka Point za Kubeba Kombe

Simba itakuwa inakibarua dhidi ya wenyeji wa mji huo, Njombe Mji FC, katika mchezo wa ligi kuu bara utakaopigwa majira ya saa 10 jioni. Njombe Mji itakuwa inaikaribisha Simba ikiwa na kumbukumbu mbaya za kuondoshwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho na Stand United ya mjini Shinyanga. Tayari timu zote mbili zimeshakamilisha maandalizi kuelekea mchezo mchezo huo wa leo.

Read More »

Yanga VS Singida United, Kesho Mtoto Hatumwi Dukani Kombe la FA

Kikosi cha Yanga kesho kitashuka dimbani Uwanja wa Namfua kwa ajili ya kucheza dhidi ya Singida United kutafuta nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali Kombe la FA. Yanga ambayo ilikuwa imeweka kambi ya muda mfupi mjini Morogoro, tayari ipo Singida huku ikielezwa wachezaji wake wote wapo fiti kiafya. Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema wachezaji ...

Read More »

Tanzania Yaombwa Kuwa Mwenyeji Kombe la Kagame

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limepokea barua kutoka CECAFA ikiomba Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Kagame kwa ngazi ya klabu. TFF imepokea barua hiyo leo ikiitaka Tanzania iwe mwenyeji wa michuano hiyo ambayo mara nyingi hufanyika jijini Dar es Salaam inapotokea Tanzania kwa mwenyeji. Kwa mujibu wa Afisa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, amethibitisha shirikisho hilo ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons