Makala

Utaratibu wa kuajiri watoto wadogo

Mtu aliye chini ya umri wa miaka 18 ni mtoto. Kisheria si kosa kumwajiri mtoto. Nataka tuelewane vizuri katika hili. Tunatakiwa kuifahamu sheria. Wengi wanadhani ni kosa kumwajiri mtoto. Wanaposikia kampeni za ajira kwa watoto wanadhani ni kosa na haramu kabisa  kumwajiri mtoto. Ndiyo maana nikasema inabidi tuelewane na tuijue sheria ili siku nyingine tunaposikia kampeni hizi tujue zinamaanisha nini. ...

Read More »

Mwalimu Nyerere angekuwepo angesemaje?

Namshukuru Mungu nimeweza kuketi kuandika kumkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kipindi hiki cha kumbukizi ya kuzaliwa kwake na kujiuliza swali ambalo bila shaka Watanzania wengine nao wamekuwa wakijiuliza: Mwalimu angekuwapo akaona utendaji wa Rais John Pombe Joseph Magufuli kwenye Awamu hii ya Tano, angesemaje? Watanzania tuliokuwapo Awamu ya Kwanza tulishuhudia uongozi uliotukuka wa Mwalimu Nyerere. Mwalimu ...

Read More »

Kutokujiandaa ni kujiandaa kushindwa

Kujiandaa ni kujiandaa kushinda na kutokujiandaa ni kujiandaa kushindwa. Rais wa 16 wa Marekani, Abraham Lincoln (1809 – 1865) anasema: “Ukinipa saa sita ili niukate mti, nitatumia saa nne za awali kuliona shoka langu.” Hii ni busara inayoonyesha umuhimu wa kujiandaa. Dunia inamilikiwa na watu waliojiandaa kuimiliki. Huwezi kuimiliki dunia bila kujiandaa kuimiliki. Eleanor Roosevelt anasema: “Wakati ujao unamilikiwa na ...

Read More »

Unaitambua nguvu ya moja?

Moja ni mtihani. Kuna nguvu ya moja. Anayefunga goli ni mtu mmoja lakini timu nzima inafurahi. Lakini kwa upande mwingine kosa la mtu mmoja linachafua picha ya kundi zima, samaki mmoja akioza wote wameoza. Kuna nguvu ya moja. Kuna uwezekano mkubwa mtu kuidharau moja. Kumbuka mdharau mwiba mguu huota tende. Kuna nguvu ya moja. Okoa shilingi moja, shilingi moja itakuokoa. ...

Read More »

Nawapongeza Mpanju, DPP Biswalo

Miongoni mwa habari zilizopewa umuhimu katika toleo hili inahusu kuachiwa huru kwa mahabusu 201 waliokuwa katika magereza ya wilaya za Musoma, Tarime na Serengeti mkoani Mara. Kuachiwa kwao ni matokeo ya ziara ya ukaguzi ndani ya magereza hayo uliofanywa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju; Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga na wadau ...

Read More »

Buriani Dk. Mengi

Kifo kimeumbwa, kifo ni faradhi. Kifo ni ufunguo wa kufunga uhai wa binadamu duniani na kufungua maisha ya milele ya binadamu huko ahera (mbinguni). Faradhi na ufunguo umemshukia ndugu yetu mpendwa, Dk. Reginald Abraham Mengi.  Reginald Mengi amefariki dunia. Ni usiku wa kuamkia Alhamisi wiki iliyopita katika Jiji la Dubai, Falme za Kiarabu, Reginald alifariki dunia baada ya kuugua kwa ...

Read More »

Yah: Malipo ni hapa hapa duniani

Salamu ndugu zangu wote mliopata baraka ya kuishuhudia Pasaka. Sina hakika, lakini ni kweli kwamba wengi walipenda kufurahia ufufuko wake Yesu Kristo mwaka huu lakini haikuwa hivyo. Wapo ambao waliweka malengo ya miezi sita na mwaka, lakini mipango yao haikuwa na mkataba wa maisha au siha njema na mipango hiyo imevurugika. Vilevile nawatakia mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ...

Read More »

Ndugu Rais tupandishe madaraja

Ndugu Rais, Mei ‘Dei’ ya Mbeya imepita. Wanaotaka kujifunza wataisoma. Lo! Maandamano yalikuwa marefu! Lo, mabango yalikuwa mengi yale, lakini yote yalibeba ujumbe mmoja unaofanana. Ulisomeka: “Tanzania ya uchumi wa kati inawezekana. Wakati wa mishahara na masilahi bora kwa wafanyakazi ni sasa.” Wafanyakazi walisisitiza nyongeza ya mishahara kwa nguvu zao zote kistaarabu. Tunasema kistaarabu kwa sababu katika nchi nyingine hali ...

Read More »

Wasaidizi, mnamsaidia?

Nianze kwa kuwatakia heri ya Pasaka pamoja na Sikukuu ya Wafanyakazi. Wiki mbili zilizopita ambazo zimekuwa na siku za mapumziko nyingi, zimenipa nafasi ya kutafakari kuhusu namna Rais Dk. John Magufuli anavyofanya kazi zake. Wiki moja kabla ya Pasaka rais alikuwa ziarani mkoani Ruvuma. Kwanza nimpongeze kwa kufanya ziara ambayo kwa hakika imeponya mioyo ya Wana Ruvuma kwa kiasi kikubwa. ...

Read More »

Rais Magufuli ‘amewaponya’ Ruvuma, Mbeya wanafuata

Ziara ya Rais Dk. John Pombe Magufuli mkoani Ruvuma imebadili mawazo ya wananchi baada ya kero zao kujibiwa lakini ikaacha majonzi kwa wananchi wilayani Songea Mjini kutokana na mkutano wa Rais kutekwa na mawaziri na kukatishwa na mvua kubwa iliyomkaribisha mkoani humo. Ikiwa ni ziara yake ya kwanza mkoani Ruvuma tangu aingie madarakani Novemba 2015, Rais John Magufuli alileta hamasa ...

Read More »

Ni demokrasia Arumeru Mashariki?

Wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanashangilia ushindi wa Jimbo la Arumeru Mashariki wa mgombea wao kupita bila kupingwa ni muhimu kwa watu makini wa taifa hili kufanya tafakuri ya nguvu juu ya matukio haya ndani ya taifa letu. Na swali la msingi ni je, tunaimarisha demokrasia katika taifa letu au tunaizika demokrasia? Au labda mifumo hii tumebambikizwa tu, si utamaduni ...

Read More »

Ndugu Rais, sasa ‘ruksa’ mtumishi akapumzike

Ndugu Rais, naandika kutoa ushuhuda ili wote wanaopitia katika majaribu magumu watambue kuwa wanaomtegemea Mungu hawatafadhaika kamwe. Alhamisi iliyopita Aprili 25, 2019 nilikuwa Ifakara High School kushiriki katika mahafali ya wahitimu wa kidato cha sita, binti yangu alikuwa miongoni mwao. Shule ile imejengwa vizuri. Zilikuwapo tetesi kuwa ilijengwa na Wacuba miaka ya 1960. Imejengwa katika mandhari na mazingira yaliyo bora ...

Read More »

Angekuwepo Mwalimu Nyerere…

Kama angekuwa hai, tarehe 13, Aprili 2019 Mwalimu Nyerere angetimiza umri wa miaka 97. Muda mfupi kabla ya hapo, nilifikiwa na ugeni wa mtu aliyejitambulisha kwanza kama ni jamaa yangu kwenye ukoo wetu lakini ambaye sijapata kuonana naye. Hilo si ajabu kwa sababu ya ukubwa wa ukoo wenyewe. Aliniletea ujumbe kutoka kwa mtu mwingine kunijulisha kuwa Mwalimu Nyerere yuko hai, ...

Read More »

Mtuhumiwa kuachiwa huru kwa ushahidi wa utambuzi

Katika Rufaa ya Jinai Namba 273 ya 2017, kati ya GODFREY GABINUS @ NDIMBA  na YUSTO ELIAS NGEMA •••..•.•.•••••.••••.•••.••••.•••• APPELLANTS Na EXAVERY ANTHONY @ MGAMBO dhidi ya JAMHURI (haijaripotiwa), hukumu ya Februari 13,  mwaka huu (2019) majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa wanaeleza kanuni tano ili ushahidi wa kumtambua mtu umtie mtuhumiwa hatiani. Lakini kabla ya hayo, ushahidi wa utambuzi ni ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (27)

Hofu ya kushindwa isizidi furaha ya kushinda   Hofu ni mtihani. Hofu ya mwanamke ni hofu ya kutumiwa na baadaye kuachwa. Hofu ya mwanamume ni hofu ya kushindwa kwenye maisha. “Palipo na hofu hakuna furaha.” (Seneca). Anayeogopa kitu anakipa nguvu juu yake (methali ya Kimoorishi). Hofu ni adui wetu namba moja. Kuna hofu za aina nyingi. Kuna hofu ya mateso. ...

Read More »

Uhuru una kanuni na taratibu zake (2)

Baada ya kutambua maana na aina ya uhuru katika sehemu ya kwanza ya makala hii, leo nakamilisha kwa kuangalia kanuni na taratibu za uhuru. Uhuru una thamani unapotekelezwa kwa kuzingatia kanuni zilizopo na kusimamiwa na taratibu zilizokubaliwa na watu walio huru. Hadhari kuwa si binadamu (mtu) tu ndiye mwenye uhuru. Wanyama, ndege na wadudu kadhalika wanao uhuru. Viumbe vyote duniani ...

Read More »

Yah: Mambo ya ziara ya rais mikoani

Salamu nyingi sana wote mliotembelewa na rais, hasa mikoa ya Kusini ambako alikuwepo kuwapa salamu na shukurani za kumchagua, lakini kubwa zaidi kuzindua na kufungua miradi ambayo kwa mujibu wa sera za chama chake waliahidi watatekeleza. Naamini mmefurahi kuona mambo yenu yanakwenda mswanu. Pamoja na ziara hiyo, kwa sisi tulioko mikoa mingine, naomba tuwe wavumilivu kidogo, naamini atapanga ziara maalumu ...

Read More »

NINA NDOTO (16)

Kuwa na nidhamu utimize ndoto yako Kama yalivyo muhimu mafuta kwenye gari, ndivyo ilivyo nidhamu kwa mtu yeyote mwenye ndoto. Nidhamu ni kiungo muhimu kwa mtu anayetaka kutimiza ndoto yake. Kuna aliyesema: “Nidhamu ni msingi wa maisha yenye furaha na mafanikio.” Ni wazi kuwa umesikia watu wengi wakitaja siri za mafanikio neno ‘nidhamu’ huwa halikosi. Vitu vinavyowafanya watu wengi wafanikiwe ni ...

Read More »

Shamba la Lyamungo mali ya KNCU – Waziri

Mvutano unaoendelea kuhusu nani mmiliki halali wa shamba la kahawa la Lyamungo baina ya Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro (KNCU) na Chama cha Ushirika wa Mazao (AMCOS) cha Lyamungo unatokana na Ofisi ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini kutochukua hatua. Hii ni kutokana na ukweli kwamba suala hilo lilikwisha kuamuliwa miaka 14 iliyopita na aliyekuwa Waziri wa Ushirika ...

Read More »

Hatua kubwa miaka 55 ya Muungano

Aprili 26, mwaka huu taifa litaadhimisha miaka 55 tangu kuasisiwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Umri huo wa miaka 55 ya Muungano si haba, changamoto na mafanikio kadhaa yamekwisha kujidhihirisha na kubwa zaidi kwa upande wa mafanikio kuimarika kwa mshikamano baina ya raia wa pande hizo mbili za Muungano. Serikali zote mbili, yaani ...

Read More »

Funzo miaka 25 mauaji ya Rwanda

Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yametimiza miaka 25. Huu ni umri wa mtu mzima na hili linajionyesha wazi kule Rwanda, asilimia 60 ya watu wa Rwanda ni vijana na wengi wao ni miaka 25 na kwenda chini. Wengi wamezaliwa baada ya mauaji haya ya kinyama. Aprili 7, 2019 Rwanda ilifungua siku mia moja za maombolezo ya kumbukumbu ya miaka 25 ...

Read More »

UJENZI GATI JIPYA LA MAGARI BANDARI YA DAR WAFIKIA ASILIMIA 50

Kazi ya utekelezaji wa ujenzi wa Gati mpya kwa ajili ya kuhudumia Meli za magari (RoRo Berth) kwenye Bandari ya Dar es Salaam imefikia asilimia 50 na ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2019. Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema mbali na kukamilika kwa ujenzi wa Gati hiyo unaotarajiwa kukamilika katikati ya 2019, kazi ya kuboresha Gati namba ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons