Makala

Wamiliki wa daladala na machozi yasiyokauka

Baada ya kununua basi dogo (Hiace) la kwanza na kulisajili daladala, nilikutana na ulimwengu mpya wa changamoto za biashara za magari. Changamoto zilipozidi niliazimu kukutana na walionitangulia kwenye biashara hiyo ili nipate hazina ya ushauri.

Read More »

Baraza la Kata Kwashemshi tupewe semina

Mimi ni msomaji wa Gazeti Jamhuri. Naishi hapa Kwashemshi wilayani Korogwe. Kinachosikitisha ni kwamba tangu mwaka jana tuteuliwe katika Baraza la Kata hakuna semina yoyote ambayo wajumbe tumepewa.   Sasa inatuwia vigumu kwetu kutafsiri sheria. Hali hii ni kinyume kabisa na utoaji haki.   Ni mimi mjumbe, Baraza la Kata, Kwashemshi, Korogwe

Read More »

Bongo: Matendo kwanza

“Ni wajibu wa viongozi wa Afrika kuonyesha utashi wao wa kisiasa, kwa ajili ya kuhakikisha taasisi za umajumui wa Kiafrika (pan-African) unakuwa chombo murua na kisiwe chombo cha mijadala isiyo na ukomo.”

Haya ni maneno ya aliyekuwa Rais wa Gabon, Omar Bongo, aliyefariki mwaka 2009 baada ya kuitawala nchi hiyo kwa muda mrefu.

Read More »

Taifa letu lipo njia panda

*Bunge, wabunge, vyombo vya habari, wananchi tujadili

Ninakumbuka baadhi ya michango ya mjadala juu ya bajeti ya mwaka 2012/2013 na jinsi ilivyokuwa ya kichama zaidi kuliko uhalisia. Wabunge wetu walisahau kabisa kusudi kubwa kati ya yaliyowaweka bungeni, yaani utashi wa nchi, kwa maana ya uwakilishi wa mamilioni ya Watanzania waliowaamini na badala yake kwa kiwango kikubwa wakatekeleza utashi wa sera za vyama vyao na utashi binafsi.

Read More »

Njooni shambani mtajirike

Miezi kadhaa iliyopita kupitia Redio TBC Taifa, ofisa mmoja wa Wizara ya Maliasili na Utalii aliulizwa swali hili, “Je, inawezekana watu binafsi kufungua mashamba ya miti na kufanya biashara ya kuuza miti ya mbao?”

Read More »

Siri zaanza kuvuja rushwa Kamati za Bunge

 

Mtandao wa wafanyabiashara wahusishwa

Kamati ya Maliasili, Mazingira yaguswa

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira aliyejitambulisha kuwa ni mpinga vitendo vya rushwa, ameamua kuandika makala hii kueleza baadhi ya vitendo vya rushwa ndani ya Kamati hiyo. Hii ni sehemu ya makala ya mbunge huyo ambaye kwa sasa tunalihifadhi jina lake.

UTANGULIZI

Tarehe 28 Julai 2012, Bunge la Tanzania liliingia katika historia baada ya Spika Anne Makinda kutangaza kuivunja Kamati ya Nishati na Madini pamoja na kamati nyingine zinazotuhumiwa kwa rushwa.

Spika alifikia hatua hiyo baada ya kuwapo kwa harakati za wafanyabiashara wa sekta ya mafuta kufanya mipango kwa zaidi ya wiki mbili za kuwashawishi wabunge washinikishe kujiuzulu kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, na Katibu Mkuu Eliakim Maswi kwa kile kinachodaiwa kutoa zabuni kwa kampuni ya Puma Energy ya kuiuzia mafuta Tanesco kwa ajili ya mitambo ya umeme wa dharura ya  IPTL. Harakati zililenga wabunge wengi wenye ushawishi bungeni, wakianzia na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya

Read More »

Kikwete: Hakuna vita

“Namhakikisha ndugu yangu, watu wote wa Malawi kwamba hatuna nia wala mpango wa kuingia vitani. Hatuna matayarisho ya Jeshi wala jeshi halijasogea popote… mimi ndiye kamanda mkuu wa jeshi na sijapanga wala kutoa maelekezo ya vita.”   Haya ni maneno ya Rais Jakaya Kikwete aliyoyasema mwishoni mwa wiki mjini Maputo, Msumbiji wakati akifanya mkutano wa pamoja na Rais Jakaya Kikwete. ...

Read More »

Je, wote tuwe wajasiriamali?

Nianze kwa kushukuru na kutambua mirejesho ya wasomaji wa safu hii ambao wanaongezeka kila wiki. Mirejesho mnayoniletea kwa ujumbe mfupi wa maandishi, kupiga simu na kuniandikia baruapepe ina thamani na umuhimu mkubwa sana katika kunogesha safu hii.

Read More »

Bunge la sasa linaelekea wapi? (2)

Duniani kote upinzani huwa una tabia ya kuchokonoa upungufu wa hoja na kisha kuonyesha vipi maboresho yangekuja kama wao wangeongoza Serikali. Hii maana yake bungeni unakuwapo ukosoaji wa aina mbili.

Read More »

Kennedy: Tusiichekee vita

“Mwanadamu anapaswa kumaliza vita, vinginevyo vita itammaliza mwanadamu.”

Haya ni maneno ya Rais wa 35 wa Marekani aliyeuawa mwaka 1963. John F. Kenney alikuwa akiamini kuwa dunia inaweza kuwa salama zaidi kwa kutoendekeza vita.

Read More »

Barua ya kibiashara kwa BRELA

Baada ya kuandika makala ya “Biashara za sasa zinahitaji u-sasa”, kuna jambo nililitazamia ambalo limetokea kama yalivyokuwa matarajio yangu. Kumekuwa na wasomaji wengi nchi nzima ambao wameleta maombi na ushauri wakitaka niwasaidie kusajili biashara zao katika mfumo wa kampuni.

Read More »

Denis Vedasto: Mjasiriamali aliyekuta na JK

“Niliona  ni vyema nikuze kipaji changu kuliko kitumike na watu wengine kwa kuajiriwa, kwani nina ubunifu mkubwa kuliko ndiyo maana niliona ni bora nianzishe kampuni yangu.” Hayo ni maneno ya Denis Vedasto, mkazi wa Kitunda, Dar es Salaam ambaye ni mjasiriamali anayejishughulisha na utengenezaji wa vitanda vya hospitali, ambavyo vingine hutumiwa wakati wa kinamama kujifungua.

Read More »

Dk. Lwaitama: Tuboreshe, tusivunje Muungano

Nimesikitishwa na aina ya uandishi wa habari  uliojiweka wazi  katika taarifa iliyonukuliwa kuandikwa na mwandishi wa gazeti moja la kila siku  (Tanzania Daima la Agosti 7, 2012), Datus Boniface.  Huyu mwandishi, pamoja na wahariri wake walioruhusu habari hiyo kuchapwa  walithubutu kusema uongo kuwa  eti “ Dk Lwaitama, Prof. Sheriff na Prof Shivji waliushambulia Muungano.” Tena, mwandishi huyu na wahariri walioruhusu habari hiyo ichapishwe  wakaenda mbali zaidi na kutumia  kichwa  cha habari kilichosema eti ‘Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe’.

Read More »

Mjue Kada wa CCM Mohsin Abdallah

 

 

*Tume ya Jaji Warioba ilianika madudu yake

*Ni bilionea anayehodhi vitalu vya uwindaji

Hivi karibuni, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) aliuibua bungeni mkataba ulioingiwa baina ya kampuni za Uranium Resources PLC, Western Metals Limited na Game Frontiers of Tanzania Limited uliotengenezwa na Kampuni ya Kitanzania ya Rex Attorneys, na kusainiwa Machi 23, 2007.

Read More »

Nyerere: Wazanzibari waamue

“Ikiwa Wazanzibari wataukataa Muungano, bila mashinikizo kutoka mataifa ya nje, siwezi kuwapiga mabomu kuwalazimisha.”

Haya ni maneno ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kueleza nia yake ya wazi kuwa ikiwa Wazanzibari wanaona hawautaki Muungano hawezi kuwazuia.

 

 

Read More »

Biashara za sasa zinahitaji u-sasa

Ingawa kuna mambo mengi hapa katika u-kisasa, kwa leo nitagusia maeneo matatu tu. Mosi, kuweka biashara katika mifumo rasmi; pili kuwa na maono; na tatu kutengeneza mfumo wa kurithisha biashara kutoka baba kwenda kwa watoto - kutoka kwa wajukuu kwenda kizazi cha pili. Biashara katika mifumo rasmi ina dhana pana, lakini kwa urahisi kabisa ni kuendesha biashara katika mifumo inayoelezeka. Ni ile hali ambayo mmiliki unapokuwapo au kutokuwapo biashara inaendelea kama kawaida.

Read More »

Hotuba iliyowazima  wabunge mafisad

Bunge linanuka rushwa. Baadhi ya wabunge wanapokea rushwa ili kutetea maslahi ya wanaowatuma. Lakini wapo wabunge jasiri walioamua kupambana na wenzao wala rushwa kama inavyothibitishwa na Hotuba ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Wizara ya Nishati na Madini, John Mnyika, kuhusu mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2011/2012 na makadirio ya matumizi ya Wizara ya Nishati na ...

Read More »

Biashara za sasa zinahitaji u-sasa

Wakati baba yangu mzazi akifariki katikati ya miaka ya 1990, alikuwa mmoja wa wafanyabiashara waliokuwa wakipanda kwa kasi kubwa kibiashara. Akiwa ameshakusanya uzoefu wa kusafiri kibiashara hadi nchi jirani ikiwamo Malawi, alifariki dunia na kuacha biashara zilizokuwa zimestawi kweli kweli.

Read More »

Ewura yaokoa bilioni 170/-

*Ni baada ya kudhibiti uchakachuaji kwa kuweka vinasaba

*Wabunge waliotemeshwa ulaji wanaanza harakati ivunjwe

 

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeliwezesha taifa kuokoa zaidi ya Sh bilioni 170 kwa mwaka, lakini hatua hiyo imewakera baadhi ya wabunge waliokuwa wakichakachua na sasa wanafanya mbinu ivunjwe.

Read More »

Hotuba ya Upinzani iliyozuiwa bungeni hii hapa

Wiki iliyopita Serikali iliibua hoja na kufanikiwa kuzuia baadhi ya maneno yaliyokuwamo kwenye hotuba ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzanji Bungeni wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Vincent Nyerere, yasisomwe. JAMHURI inakuletea hicho kilichozuiwa kusomwa.

Read More »

Siri ya mafanikio yangu kiuchumi – 2

Wiki iliyopita nilieleza namna changamoto za kiuchumi zinavyowahenyesha wafanyakazi. Pia nilianza kueleza mchapo unaonihusu wa namna nilivyopambana kujikwamua kiuchumi nikiwa nimeajiriwa kwa kazi ya ualimu. Leo nitahitimisha kwa kubainisha mbinu kadhaa ili kumudu mchakamchaka wa maisha ya kiuchumi. Endelea...

Read More »

Museveni: Waafrika hatujui kuomba

“Tatizo letu sisi Waafrika hatujui kuomba, na hata tunapopata fursa ya kuomba hatuombi kwa akili. Nilipokwenda kwa Gaddafi [wakati napigana vita ya kumuondoa Idi Amin) aliniuliza ‘Nikupe pesa?’ Nikasema hapana. Akasema ‘Nikupe sare za askari?’ Nikamwambia hapana. Akasema ‘Unataka nini sasa kwangu?’ Nikamwambia bunduki na risasi.”

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons