Wakati baadhi ya mataifa yakijiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), baadhi ya ligi za barani Ulaya zitawakosa nyota wake wanaotoka barani Afrika. Ligi ya Uingereza pekee itawakosa wachezaji 26.

Fainali hizo za AFCON zitaanza kutimua vumbi Januari 14, mwaka huu nchini Gabon.

JAMHURI inakuletea baadhi ya majina ya wachezaji watakaozikosa baadhi ya mechi za Ligi Kuu ya Uingereza wakati wa fainali za AFCON. Klabu nyingi Ulaya zitaathiriwa na fainali hizo.

Wachezaji wanatarajiwa kuingia mapema kambini ili kujiandaa na fainali hizo. Hivyo wataziacha timu zao kutoka katika Ligi Kuu ya Uingereza na kwenda kuungana na wachezaji wenzao kutoka klabu mbalimbali duniani.

Klabu ya Arsenal itamkosa kiungo wake Mwarabu, Mohamed Elneny kutoka (Misri), Bournemouth: Max Gradel (Ivory Coast), Benik Afobe (DR Congo), Crystal Palace: Wilfried Zaha (Ivory Coast), Bakary Sako (Mali). Everton: Idrissa Gueye (Senegal), Hull City: Ahmed Elmohamady (Misri), Dieumerci Mbokani (DR Congo), Leicester City: Riyad Mahrez (Algeria), Islam Slimani (Algeria), Daniel Amartey (Ghana), Jeffrey Schlupp (Ghana), Liverpool: Sadio Mane (Senegal), Man United: Eric Bailly (Ivory Coast), Southampton: Sofiane Boufal (Morocco), Stoke City: Wilfried Bony (Ivory Coast), Mame Biram Diouf (Senegal), Ramadan Sobhi (Egypt).

Klabu nyingine zinazoshiriki Ligi Kuu Uingereza zitakazoathiriwa ni pamoja na Sunderland (Uingereza), Wahbi Khazri (Tunisia), Lamine Kone (Ivory Coast), Didier Ndong (Gabon), Watford: Nordin Amrabat (Morocco), Adlene Guedioura (Algeria), West Ham: Andre Ayew (Ghana), Sofiane Feghouli (Algeria), Cheikhou Kouyate (Senegal).

Muonekano wa timu na makundi AFCON 2017.

KUNDI A kuna timu za Gabon, Burkina Faso, Cameroon na

Guinea Bissau.

KUNDI B  kuna Algeria, Tunisia, Senegal na Zimbabwe.

KUNDI C kuna Ivory Coast, DR Kongo, Morocco na Togo.

KUNDI D kuna Ghana, Mali, Misri na Uganda,

 Wafungaji bora wa muda wote wa mashindano hayo ni

1. Samuel Eto’o – Cameroon – magoli 18

2. Laurent Pokou – Ivory Coast – magoli  14

3. Rashi Yekini Nigeria – magoli 13

4. Hasan El-Shazly – magoli 12

5. Patrick Mboma – Cameroon – magoli 11

6. Hossam Hassan – Misri  – magoli 11

7. Didier Drogba – Ivory Coast – magoli 11

8. Ndaye Mulamba – DRC – magoli 10

9. Joel Tiehi – Ivory Coast – magoli 10

10. Mengistu Worku – Ethiopia – magoli 10

11. Francileudo Santos – Tunisia – magoli 10

12. Kalusha Bwalya – Zambia – magoli 10

1144 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!