Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ya mwaka 1967 pamoja na marekebisho yake ikisomwa na muundo wa shughuli za Baraza (Provisions of the Schedule to the Act), amemteua Bw. Leodger Chilla Tenga kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa.

Dkt. Mwakyembe amewateua pia wajumbe wapya sita (6) wa Baraza hilo kama ifuatavyo:

  1. Mkumbwa M. A. Mtambo.
  2. Beatrice Singano.
  3. Kanali Mstaafu Juma Ikangaa.
  4. John Joseph Ndumbaro.
  5. Rehema Sefu Madenge.
  6. Salmin Kaniki.

Aidha, Dkt. Mwakyembe amewateua wajumbe wengine watatu (3) wa Baraza kutokana na nafasi za vyeo vyao ambao ni:

  1. Yussuph Singo – Mkurungezi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
  2. Edicome Shirima- Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi.
  3. Mohammed Kiganja, Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa ambaye atakuwa ni Katibu wa Baraza.

Uteuzi wa wajumbe wote umeanza rasmi tarehe 08 Februari, 2018 na watalitumikia Baraza kwa kipindi cha miaka mitatu (3).

Vilevile Dkt. Mwakyembe kwa mujibu wa sheria amemteua Bw. Timothy Mganga kuwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kwa kipindi cha miaka mitano (5).

Imetolewa na;

Lorietha Laurence

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.

09/02/2018

By Jamhuri