Trump anaamini Parscale atasaidia kushinda tena kiti cha urais
Trump anaamini Parscale atasaidia kushinda tena kiti cha urais
Brad Parscale anatajwa kuwa amebobea vilivyo katika masuala ya mitandao
Brad Parscale anatajwa kuwa amebobea vilivyo katika masuala ya mitandao

Rais wa Marekani Donald Trump amemtaja meneja wa kampeni zake za urais mwaka 2020.

Brad Parscale mtaalam wa mitandao, alifanya kazi katika kampeni za Trump 2016 na alisifiwa sana kwa kutumia mitandao ya kijamii vizuri jambo linalotajwa kumpa ushindi Trump.

Parscale atatumika katika kampeni za uchaguzi mdogo baadae mwaka huu.

Trump anasema Parscale ni mtu sahihi na amekuwa akifanya kila kitu kwa uhakika wa hali ya juu.

By Jamhuri