Korea Kaskazini imekuwa ikiwatumia vifaa Syria ambavyo vinaweza tumika katika kutengeneza silaha za kemikali, ripoti ya chombo cha habari Marekani imesema kikinukuu ripoti kutoka Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa ripoti ya UN ambayo haijatolewa, wataalam wa bakora Pyongyang wameonekana katika viwanda vya kutengenezea silaha nchini Syria, gazeti la New York Times imesema.

Shutuma hizo zinakuja baada ya ripoti mpya ya utumiaji wa gesi ya chlorine na vikosi vya Syria, shutuma hizo zimekanushwa na serikali.

Korea Kaskazini ipo chini ya vikwazo vya kimataifa sababu ya programu yao ya nuklia.

Vifaa hivyo vinaripotiwa kupatikana kiwizi na kutumwa Syria na Korea Kaskazini vikiwemo vigae venye uwezo wa kuzuia joto na tindi kali mwingi na vipima joto. Vigae vinasemekana kutumika katika kujenga majengo ambapo silaha za kemikali zitatengenezwa.

Inasemekana wamtumiwa makumi ya mizigo ndani ya miaka kadha.

Gazeti hilo linasema, taasisi ya utafiti ya maswala ya sayansi ya Syria inasemekana kuwalipa Korea Kaskazini kupitia makumpuni bandia.

By Jamhuri