Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema hakuna sheria kuwakamata watu wanaovaa nguo fupi au kwa wanyoa viduku sisi kazi yetu ni kusimamia sheria na mimi siwezi kufanya kazi nje utaratibu wa sheria za nchi.
Lakini endapo Bunge italitungia sheria suala hili, basi mimi nitasimamia kuhakikisha sheria haivunjwi.’ Mambo Sasa alisema.
Aliendelea kusema. ‘Hili suala la Kuzuia vimini na viduku limezushwa, Mimi niliitisha Press kuelezea mafanikio ya Jeshi la Polisi Kwa kanda maalum Kwa kipindi hiki cha sikukuu kilichopita.
Na hili swali niliulizwa nikasema kuwa linavunja maadili na huu si utaratibu wetu ni watu wa magharibi si maadili yetu kabisa lakini kwetu bado sio kosa kisheria. Lakini kama watu hao watajihusisha na ukahaba basi hapo watakuwa wametenda kosa la Jinai hivyo hawatasita kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vinavyohusika ili sheria ichukue mkondo wake.

SOURCE:  CLOUDSFMTZ Power Breakfast.

1516 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!