Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA, kanda ya Zanzibar, imewatoa wasiwasi wamiliki wa tovuti, blogi, redio na televisheni za mtandaoni, kuwa usajili utashughulikiwa na Tume ya Utangazaji Zanzibar na sio TCRA.

Hayo yanakuja kufuatia tangaazo la hivi karibuni la TCRA, la kuwataka wamiliki wa mitandao hayo kusajili haraka vyinginevyo hawataruhusiwa kutoa huduma.

Baadhi ya mitandano, ukiwemo mtandao maarufu wa Jamii Forum, umesitisha kutoa huduma kutokana na tangazo hilo la TCRA.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Meneja wa TCRA kanda ya Zazibar, Esuvatie Aisa Masinga, alisema wamiliki wa mitandao hiyo waliopo Zanzibar, wasiwe na wasiwasi kwamba watawajibika kwa TCRA kama wengine wanavyofikiria.

Alisema waendelee kufanya kazi zao kwa ufanisi na wala wasiwe na wasi wasi kwamba TCRA itaingilia kati.

 

By Jamhuri