Wakati wakulima wa korosho wanaanza
kufaidi – (kwa Kimwela ‘kupoka’) neema za
korosho, mara mwaka ule wa 1973 serikali
ikavunja ile bodi ya mazao, lakini ikaunda
mamlaka maalumu kwa zao letu la korosho.
Mamlaka hiyo ilijulikana kama CATA
(Cashew Authority of Tanzania).
Majukumu ya mamlaka hii yalikuwa kuweka
bei za korosho, kununua na kuuza korosho.
CATA ilishughulikia kikamilifu zao la
korosho, kupanga bei, kununua korosho,
kuzi-grade kuzisafirisha na kuziuza nje ya
nchi. (Angalizo: moja ya alama ya ufanisi
wa CATA ni yale majengo kama ‘CATA
Club’ na majumba ya watumishi yaliyopo
pale Mtwara).
CATA waliweza kukusanya korosho kutoka
unions zote na kuzipeleka Mtwara kwa

mauzo. CATA walizihudumia pia barabara
za wilayani kwenda vijijini zinakonunuliwa
korosho za wakulima. Ndiyo sababu kutoka
mwaka 1960 – 1972, korosho zote
zilinunuliwa kutoka kwa wakulima na
kuuzwa kwa wafanyabiashara wa nje kwa
pamoja.
Utaratibu huu ulionekana kufanikiwa kwa
sababu kule India nako kuliundwa chama
kilichoitwa ‘The Cashew Corporation of
India’ kilichopewa jukumu la kununua
korosho ghafi kutoka nje na kuwauzia
wenye viwanda vya ubanguaji kule India.
Shirika hilo lilikuwa na makao makuu yake
katika mji wa Cochin, Jimbo la Kerela.
Uhusiano ulikuwa kati ya NAPB na Cashew
Corporation of India.
Kwa njia ya NAPB baadaye ikawa CATA,
ndiye alikuwa mnunuzi pekee wa korosho
za wakulima na ‘exporter’ pekee wa
kuzipeleka nje (buyer and exporter).
Korosho zote zilitiwa katika madaraja, na
India ilileta wataalamu wake kufunza
wananchi namna ya kupanga madaraja ya
korosho. Basi kila penye ‘union’ palikuwa na

mtu anayepanga madaraja ya korosho.
Wahindi walizichambua korosho zetu na
kuzipanga kiubora, zile za Tunduru, Masasi
na Nachingwea, kundi lake, (walizitambua
kama CD, KL) wakati zile zilizotoka Newala
na Mtwara waliweka kundi lake na
(kuzitambua kama AFGHI); wakati korosho
kutoka pwani ya Lindi, Kilwa na Dar es
Salaam zilitiwa katika kundi lake
(zikatambulika kama BE). (NB. Maana ya
herufi hizo sizijui) la muhimu ni kuwa
korosho zote zilipangwa kwa daraja la
kwanza (I) au ‘standard grade’ na daraja la
II au ‘under grade’.
Kwa ujumla korosho zetu zilikuwa bora
kuliko zile zilizotoka nchi jirani ng’ambo ya
Mto Ruvuma. Zote ziliuzika, kadiri miaka
ilivyopita ndivyo zao la korosho liliongezeka
kwa wingi katika nchi hata serikali
ikashawishika kujenga viwanda vya
kubangulia korosho zetu kwa kujipatia
kipato zaidi.
Msimu wa mwaka 1973/1974 tani 110,000
za korosho zilivunwa na kuuzwa zote.
Mwaka 1974 serikali ilitafuta mtaji kutoka

Benki ya Dunia – mkopo wa kujengea
viwanda vya kubangua korosho.
Uchambuzi yakinifu uliotolewa wakati ule
ulikubaliwa na Benki ya Dunia kuwa zao la
korosho likibanguliwa humu nchini
kutakuwa na faida kubwa kiuchumi.
Basi, serikali ilipanga kujenga viwanda kwa
awamu mbili. Awamu ya kwanza viwanda
vijengwe Lindi (tani 10,000), Masasi (tani
10,000), Newala (tani 10,000), Mtama (tani
5,000) na Nachingwea (tani 5,000).
Awamu ya pili ilikuwa vijengwe Tunduru
(tani 10,000), Newala II (tani 10,000),
Mtwara (tani 10,000) na Masasi II (tani
5,000) baada ya vile viwanda vya awamu ya
kwanza kuonyesha mafanikio yake katika
ubanguaji.
Baada ya mipango hiyo mizuri yote
kukamilika katika makaratasi kumetokea
nini hadi leo tuko hoi watu wa Kusini?
Korosho zetu haziuziki, viwanda vyetu
vimekuwa magofu (white elephants –
wasemavyo Waingereza) hata watalii
hawavutiwi kuyatembelea? Hali ya

wakulima sasa inakuwa mbaya hata kulipa
karo za shule hawawezi. Korosho
mkombozi wa Kusini kulikoni? Mimi ninaona
mambo kadhaa yamesababisha nchi kufikia
hapo hivi sasa.
Pamoja na nia njema hiyo ya serikali
kuhimiza zao la korosho na kutaka
zibanguliwe katika viwanda vyetu ili
wakulima wafaidi bei nzuri kwa korosho
zao, nia hiyo njema bila vitendo kabambe
haitufikishi popote kiuchumi.
Ninazo sababu tatu ambazo nafikiri
zimezorotesha uchumi utokanao na
korosho.
Mosi, ile Sera ya Vijiji vya Ujamaa ya
mwaka 1974 ilirudisha nyuma zao korosho.
Mashamba kadhaa kule Kusini yaliachwa
porini, wenyewe walipohamishiwa kwenye
vijiji vipya vilivyopangwa na serikali.
Mikorosho iliungua moto, maana
mashamba yale hayakupaliliwa, hivyo
korosho hazikuzaa vizuri tena. Hii
ilisababisha zao la korosho liporomoke
kutoka mavuno ya tani 117,486 msimu wa
1974/1975 hadi tani 83,738 msimu ule wa

1975/1976. Hizi ni tani zaidi ya 33,000.
Pili, mwaka 1975 serikali ilivunja vyama vya
ushirika tulivyoita ‘unions’ ambavyo vilikuwa
mahali maalumu pa kuuzia korosho za
mkulima. Serikali iliamua vijiji vya ujamaa
ndivyo vinunue korosho. Vijiji vyenyewe
havikuwa na uwezo kifedha, havikujiandaa
kwa ununuzi mkubwa namna hiyo, na yale
mabenki yaliyokuwa yanakopesha ‘unions’
hayakuwa tayari kukopesha vijiji vya
ujamaa. Katika hali namna hii, korosho za
mkulima hazikununulika ilivyotazamiwa.
Tatu, ule mpango wa kwanza uliokubaliwa
mwaka 1974 wa kujenga viwanda kwa
awamu mbili haukufuatwa. Waroho
waliishauri serikali viwanda vyote vijengwe
kwa wakati mmoja huo huo ingawa waliona
zao la korosho linaporomoka.
Isitoshe watu walikuwa wamekiuka lile
sharti la kusema tuone viwanda vya kwanza
vinabangua namna gani, lakini kabla ya
kupata mrejesho wa ufanisi huo, waroho
wakaishauri serikali iendeleze ujenzi wa
viwanda ile awamu ya pili. Huku ni
kumfanya mtoto ajitahidi kukimbia wakati

hata hajaweza kusimama na kuanza
kutembea! Hili lilikuwa kosa kubwa sana
kiutendaji.
Inaonekana basi serikali ingawa iliona
uzalishaji wa korosho unaporomoka, ujenzi
wa viwanda unaongezeka kiholela, mabenki
hayakuweza kukopesha vijiji vya ujamaa
kama yalivyofanya kwa ‘unions’

, lakini

hakuna hatua thabiti zilizochukuliwa wakati
ule kuzuia hayo yasitokee, hivyo
kuwahakikishia wakulima kipato cha jasho
lao.
Miaka ile ya 1980 na mwanzoni mwa miaka
ya 1990 uzalishaji wa korosho ulizidi
kudorora. Serikali mwaka 1984 ilibadilisha
ile mamlaka ya korosho na kuwa Bodi ya
Korosho Tanzania – Tanzania Cashewnut
Marketing Board (TCMB). Bodi hii bado
haikuweza kuliendeleza zao hili la korosho.
Basi, katika mparaganyiko namna hii, kila
kitu kinaweza kutokea na kila mtu anaweza
kubwata lawama zake.
Baadhi ya wafanyabiashara wenye kujiweza
kifedha (labda kwa baraka za Wizara ya
Kilimo) walianzisha chama cha wanunuzi

wa korosho wakakiita Umoja wa Korosho
Tanzania (CBAT) (Cashewnut Buyers
Association of Tanzania). Umoja huu ulibuni
mfuko wa kuendeleza zao la korosho
ulioitwa CIDEF (Cashenuts Industry
Development Fund) ili uwasaidie katika
azma yao ya kununua korosho kiulaini.
Wafanyabiashara wote ulimwenguni wana
tabia ile ile ya kununua vitu kwa bei ya chini
kisha kuuza kwa bei ghali. Mipango
ikasukwa hadi wizarani ambako
kulianzishwa kitengo maalumu cha
uendelezaji korosho kilichoitwa CMU
(Cashew Management Unit). Kutoka mwaka
1994 mpaka mwaka 2000 wafanyabiashara
walijaribu sana kuonyesha kuwa wao ndio
mkombozi wa zao la korosho, na wao wana
uchungu na wakulima na watasaidia kwa
hali na mali.
Mimi ninaamini hiyo ilikuwa ni ‘janja ya
nyani tu’

, maana kuna usemi wa Kiingereza

juu ya kilio cha mamba kuwa ‘shading
crocodiles tears’ – yaani kutokwa machozi
kwa mamba akamatapo windo lake.
Mwenye usongo na korosho katika nchi hii

ni mkulima.
Kule India nako lile shirika la Cashew
Corporation of India lililonunua korosho zetu
zote lilishavunjwa. Hivyo, wanunuzi binafsi
walikuwa wanajinunulia korosho kiholela
kwa viwanda vyao vya kubangulia korosho.
Wakati wa vurugu za namna hii serikali yetu
ikaruhusu soko huria kwa korosho! Matajiri
wale wa India wakawatumia mawakala wale
wafanyabiashara wa umoja wa korosho
hapa kwetu.

…..tamati…..

By Jamhuri