Wiki hii nimelazimika kuandika tena mada hii. Nimeiandika mada hii baada ya kuona moto unazidi kusambaa nchi nzima. Tatizo lilianzia Kanda ya Ziwa kwenye mikoa ya Mwanza na Geita, likaenda Shinyanga, lakini sasa limehamia Tunduma.

Taarifa nilizopata zinasema siku ya Pasaka, Kanisa Katoliki Mwanza lilichinja ng’ombe saba. Tunduma nao walichinja ng’ombe saba. Msisitizo wa Wakristo hawa ni ule wa Agano la Kale. Kwamba zilikuwa walikuwa wanachinjwa mbuzi na ng’ombe kama sadaka ya kutekelezwa, bila kuwapo Waislamu.

Historia inaonesha kuwa Uislamu ulianza miaka 610 baada ya Kristo kuja duniani. Wala sitajielekeza huko, ila najiuliza na najaribu kufikiria kwa sauti, kuwa kabla ya kuja kwa Uislamu nani aliyekuwa anawachinjia Wakristo? Kama walikuwa wanakula hivyo vinavyoitwa vibudu, je, vinaua?

Sitanii, kama vibudu vingekuwa vinaua, basi hadi inatimu hiyo miaka 610 duniani kungebaki miti na nyasi, na pengine Wahindi wachache wasiokula nyama maishani mwao. Mimi ni Mkristo, na ninapoandika makala haya bado naamini kuwa “kila kiingiacho kinywani hakimtii mtu unajisi isipokuwa kimtokacho.”

Hata hivyo, ukiacha hayo, naamini tunalo tatizo kubwa. Ibara ya 19 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa uhuru wa kila mwananchi kuabudu dini aipendayo. Viashiria ninavyoviona hapa kwenye mjadala na mgogoro unaoendelea, ni visasi na kutishiana.

Nasema ni visasi na kutishiana kwa maana kwamba Waislamu wanataka Katiba mpya ijayo itamke wazi na kutambua kuwapo kwa Mahakama ya Kadhi. Najaribu kufikiri kwa sauti kuwa huenda hata Wakristo wanaona sasa kwa kuwa Waislamu wanadai Mahakama ya Kadhi, basi nao wadai haki ya kuchinja.

Mawazo yananituma kuwa tatizo tulilonalo katika hili ni ulegelege katika kusimamia sheria. Hakuna uthabiti katika kusimamia sheria. Ndiyo maana kuna makanisa yaliyochipuka kama uyoga, na kazi yao ni kutukana Wakristo wenzao eti hawajaokoka na hivyo ni wafuasi wa shetani.

Ndiyo maana kuna misikiti inaendesha harakati na mihadhara uchwara ya kutukana imani ya dini nyingine kama Ukristo, wakidiriki kusema hadharani kuwa Yesu si Mungu. Nimefurahi baada ya wafuasi wa Sheikh Ponda Issa Ponda kuswekwa lupango kwa mwaka mzima, kutokana na vurugu walizofanya Mbagala kuchoma makanisa.

Hii itarejesha adabu. Enzi za Mwalimu Nyerere, wala tusingesikia chokochoko hizi. Alisema wazi kuwa “Nchi yetu haina dini.” Hii ndiyo iliyokuwa kauli thabiti ya Serikali. Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, zilipozuka vurugu za maduka ya nguruwe Kinondoni, alisema msimamo wa Serikali nchi haina dini. “Atakayetaka kula nguruwe ruksa, atakayetaka kula mjusi ruksa.”

Sitanii, misimamo hii miwili ya Nyerere na Mwinyi ilidumisha amani ya nchi hii. Leo tunaelezwa kuwa kuchinja ni Ibada kwa Waislamu. Nilitaraji Serikali isimame na kusema – tena kwa sauti – kuwa “NCHI YETU HAINA DINI.” Hili tu lingehitimisha mgogoro unaoendelea, mengine yakabaki kuwa siri ya jamii (social secret).

Ukiacha ukosefu wa kauli thabiti ya Serikali, naona kila dalili kuwa tunaelekea mkondo wa Ulaya na Marekani. Wanywaji na walevi, hawachagui kachinja nani. Naamini pia ‘wachinjaji’ hawana hamu ya kwenda baa kuangalia nani kachinja na nini kinaliwa, maana kwa Mwislamu swafi ni haramu kunywa pombe.

Hali hii iliwafikisha Wamarekani, Waingereza na mataifa mengi ya Ulaya kuwa na bucha zenye kuuza nyama inayojulikana kama Halal Meat. Mwislamu anayetaka kufuata masharti, anaingia kwenye bucha iliyojinasibu kuwa kachinja Mwislamu na kununua nyama yake.

Hofu yangu kuu ni kwamba hapa kwetu tukiruhusu kuwapo kwa bucha mbili, yatajitokeza madai mengine. Waislamu wataacha kwenda kwa Wakristo kwa hofu ya kula chakula kilichopikwa kwa kutumia sufuria iliyowahi kupika ‘haramu’, hata kama imesafishwa na nyama ikanunuliwa mbele ya Mwislamu kwenye bucha ‘halal’.

Sitanii, kutokana na yote hayo tuamue kama taifa, kuwa kuanzia sasa asiwepo aliyehalalishwa na chombo chochote kuchinja. Pili atakayetaka kuchinja achinje, ila asitoe tangazo la kutamba kuwa kachinja. Tubaki kama ilivyokuwa awali (siri ya jamii). Mwisho, Katiba mpya iwe na ibara inayotamka hivi: NCHI YETU HAINA DINI.

1283 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!