Baada ya kutia kandarasi ya mwaka mmoja na Mbao FC, uongozi wa Lipuli wasema wanatambua kuwa kocha Amri Said ‘Stam’ bado ana mkataba na timu yao.

Mwenyekiti wa Lipuli, Ramadhani Mahano, amefunguka na kusema wao wanatambua kuwa Stam ni kocha wao huku akisema hawajapata taarifa rasmi za kuondoka kwake.

Wakati Stam akiondoka Lipuli, kocha huyo alieleza kuwa tayari ameshaagana na mabosi wake hao wa zamani kwa kila kitu mpaka ikafikia hatua ya kujiunga na Mbao ya jijini Mwanza.

Kutokana na tukio hilo kutokea, Mahano amefunguka na kueleza wao hawatambui kuondoka kwa kocha wao ambaye amemuachia benchi Suleiman Matola peke yake.

Stam ameondoka Lipuli aliyoiongoza kumaliza ligi msimu wa 2017/18 ikiwa imeshika nafasi ya 7 sambamba na kujikusanyia alama 38.

1909 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!