Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya inaendelea tena leo usiku ambapo Liverpool watakuwa wanaikaribisha AS Roma kwenye Uwanja wa Anfield.

Liverpool waliingia hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa Manchester City kwa jumla ya mabao 5-1.

AS Roma nao walitinga hatua hiyo kwa kuifunga FC. Barcelona.

Mechi hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka duniani, itaanza majira ya saa 3 na dakika 45 za usiku.

Mechi Nyingine itachezwa kesho kwa kuwakutanisha Bayern Munich dhidi ya Real Madrid kutoka Spain.

 

2096 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!