MAAGIZO 5 YA WAZIRI MHAGAMA KWA PROGRAMU YA MIVARF KUOGEZA THAMANI YA BIASHARA ZA MIFUGO WILAYANI LONGIDO

Waziri wa Nchi Ofisi  ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge, Ajira ,Kazi,  Vijana na Watu wenye Ulemavu ) Mhe.Jenista Mhagama ameielekeza Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF), kuongeza Thamani Biashara za Mifugo wilayani Longido kwa kutatua  kero zote  za wafanyabiashara wa mifugo wilayani humo.

Mhagama ametoa maagizo hayo baada ya kukagua  Soko la kimkakati lililojengwa na Serikali kupitia Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF). Soko hilo litawanufaisha wananchi wapatao 14,2000  wa wilayani Longido ambapo asilimia 95 ni wafugaji na wanaojishughulisha na biashara za mifugo.

Soko  hilo la kimkakati ambalo halijafunguliwa rasmi , tayari halmashauri ya wilaya hiyo imeweza kukusanya mapato ya kiasi cha shilingi milioni 106 kwa mwaka  2016/2017 ambapo kwa makusanyo hayo yamewezesha halmashauri hiyo kuvunja rekodi ya miaka kumi iliyopita kwa kukusanya shilingi bilioni 1.3 kwa mara ya kwanza  kwani awali mapato yake yalikuwa chini ya bilioni moja. Aidha umuhimu wa soko hiloumejidhihirisha pale Halmashauri ilivyoweza mwezi Novemba kutoa asilimia 10ya mapato yake kwa wananwake na Vijana ikiwa nikwa asilimia5 kwakilakundi na hii ikiwa nimara ya kwanza kwa Halmashauri hiyo kuweza kutekeleza hilotangu kuanzishwa kwake.

MIVARF;  ni Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko na Huduma za Kifedha Vijijini  iliyobuniwa  na serikali ya Tanzania  kwa  kushirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo yaani (IFAD) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).   Programu hii inatekelezwa  katika mikoa 29 ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani  tangu mwaka 2011.