Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano wamekamatwa tena leo baada ya muda mfupi kufutiwa mashtaka ya kusambaza dawa feki za kufubaza makali ya ukimwi (ARV) na kujipatia Sh milioni 148 kwa njia ya udanganyifu.

Madabida na wenzake wamefutiwa mashtaka hayo katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, na baada ya kukamatwa atasomewa mashtaka mapya.

1331 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!