Rais mstaafu Aly Hassan Mwinyi amemtembelea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

Rais Mwinyi akiambatana na mkewe na maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Kenya, wamemtembelea Lissu hospitalini hapo alipolazwa tangu Septemba 7  anakotibiwa baada ya kuuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma.

Rais Mwinyi anakuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa Serikali waliomtembelea Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ambaye hivi karibuni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan naye alifika hospitalini hapo kumjulia hali.

By Jamhuri