Hatimaya Mapingwa watetezi,Yanga SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuibamiza Stand United mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 46 baada ya kucheza mechi 21.
Yanga sasa wanalingana kwa pointi na vinara wa muda mrefu msimu huu, Simba SC ingawa mabingwa hao watetezi wamecheza mechi moja zaidi.
Katika mchezo wa jana, mabao ya Yanga SC yamefungwa na beki wa Stand United, Ally Ally aliyejifunga, kiungo Ibrahim Ajib na mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa.

By Jamhuri