Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, baada ya kuwasili kwenye Mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania mjini Singida ambapo alikuwa mgeni rasmi, Novemba 30, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika mjini Singida Novemba 30, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu hicho na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (mwenye miwani mbele) akiwa na wahitimu wenzake katika Mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika mjini Singida, Novemba 30, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akimtunuku Shahada ya Uzamili Katika Elimu ya Utawala, Mipango na Sera (Master Of Education in Administration, Planning and Policy Studies), Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (kushoto) katika Mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika mjini Singida, Novemba 30, 2017. Wapili kulia ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Watatu kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinoloji, Profesa Joyce Ndalichako. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akitelemka kutoka kwenye jukwaa baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamili Katika Elimu ya Utawala, Mipango na Sera (Master of Education in Administration, Planning and Policy Studies) na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Waziri Mkuu MStaafu, Mizengo Pinda (kulia) huku Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akipokea ua kutoka kwa mwanae, Saad Majaliwa Kassim baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika Elimu ya Utawala, Mipango na Sera (Master of Education in Administraion, Planning and Policy Studies) katika Mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika mjini Singida Novemba 30, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

2677 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!