Klabu ya Arsenal ikiwa katika Uwanja wake wa nyumbani, imekubali tena kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa ligi.

Arsenal iliingia na kumbuku za kupoteza mchezo uliopita kwa kufungwa idadi ya mabao yaleyale, huku matarajio ya mchezo dhidi ya Manchester City yakiwa ni kulipiza kisasi japo matokeo yameenda sivyo.

Wafungaji wa mabao hayo ni Sane, Bernado Silva na Diego Silva.

Manchester City sasa imezidi kujiweka kileleni mwa msimamo wa Ligi kwa kufikisha alama 75 kwenye nafasi ya kwanza huku Arsenal ikiwa nafasi ya 6 na alama 45.

1842 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!