Mshambuliaji wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo, amefunguka na kueleza kuwa mkataba wake na klabu yake unamalizika Julai 7 2018.

Wakati mkataba wake ukielekea kumalizika, Mavugo amesema Yanga ni moja ya timu zinazomuwinda hivi sasa kwa ajili ya kukiboresha kikosi chake.

Mbali na kuhusishwa na Ssimba, Mavugo pia amesema ataendelea kuitumikia klabu hiyo kutokana na namna ilivyomlea tangu ajiunge na wekundu hao wa Msimbazi endapo watamuongezea mkataba mwingine.

Aidha, timu za Singida United na Gor Mahia FC ya Kenya nazo zipo kwenye rada ya kutaka kumsajili mchezji huyo kwa ajili ya huduma ya msimu ujao.

Mavugo ameeleza kwa sasa yupo nchini kwao kwa ajili ya kukitumikia kikosi cha timu yake ya taifa katika mashindano ya kufuzu kuelekea AFCON.

2139 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!