Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Uchaguzi Mdogo wa

Madiwani 43 uliofanyika Jumapili umevurugwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimkakati,

hivyo baadhi ya maeneo wamemua kujitoa ikiwamo Mkoa wa Manyara.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe (pichani) ameliambia JAMHURI kuwa zamu hii CCM wametumia mbinu ya kuanzisha utaratibu wa kuwapa barua maalum za utambulisho mawakala wa vyama, ambapo wale wa upinzani wamepewa barua hizo za utambulisho kwakuchelewa na CCM wakatumia mwanya huo “kucheza na kura”.

 

Na Deodatus Balile/JAMHURI MEDIA

1487 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!