Ligi Kuu Ubelgiji msimu wa 2019/20 imeendelea tena jana club ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilikuwa nyumbani Luminus Arena kucheza game yake ya 9 ya Ligi Kuu dhidi ya Zulte Waregem.

Game hiyo ilikuwa na mvuto wa kipekee kwani Genk ndio inacheza kwa mara ya kwanza dhidi ya nahodha wake wa zamani aliyeihama timu hiyo na kujiunga na Zulte Waregem msimu uliopita Thomas Buffel, Genk wakiwa nyumbani wamefanikiwa kupata ushindi wa 4-0.

Goli la kwanza la Genk lilifungwa na nahodha wao wa sasa Pozuelo dakika ya 29 na baadae kufuatia na hat-trick ya Mbwana Samatta aliyefunga magoli matatu dakika ya 31, 68 na 86 na kuifanya Genk kufikisha jumla ya point 23 wakiwa nafasi ya pili nyuma ya Club Brugge wanaoongoza kwa point 25.

Genk msimu huu katika game zao tisa za Ligi Kuu hawajapoteza mchezo hata mmoja zaidi ya kushinda game 7 na kutoka sare game mbili, hivyo inawaweka pazuri zaidi katika kuwania Ubingwa, kwa upande wa Mbwana Samatta leo anakuwa kafunga hat-trick yake ya pili toka ajiunge na Genk.

Hat-trick ya kwanza aliifunga dhidi ya Brondby IF katika mchezo wa kuwania kucheza Europa League msimu wa 2018/19 hatua ya makundi, hata hivyo katika Ligi Kuu, Samatta jana alifikisha jumla ya magoli manne akiwa kacheza game nane, Samatta yupo nafasi ya nne kwa wanaoongoza kwa magoli Ligi Kuu Ubelgiji msimu huu ila nafasi ya nne amefungana na wachezaji wengine tisa.

By Jamhuri