Jumamosi ya September 29 2018 club ya Man United ilikuwa London kucheza game yake ya ya Ligi Kuu England dhidi ya wenyeji wao West Ham United katika uwanja wa London Stadium.

Man United ambayo ipo katika wakati mgumu kwa sasa huku ikihusishwa kutaka kumfuta kazi kocha wake Jose Mourinho kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo,ilikubalii kipigo chake cha tatu EPL msimu katika game zake saba ikishinda tatu na kutoka sare moja.

kwa matokeo hayo Man United wamejikuta wakikubali kipigo cha magoli 3-1 dhidi ya West Ham United magoli ya West Ham United yalifungwa na Felipe Anderson dakika ya 6, Lindelof kwa kujifunga dakika ya 43 na Arnautovic dakika ya 74, goli pekee la Man United lilifungwa na Marcus Rashford dakika ya 74.

Ushindi huo wa West Ham United unaweka kibarua cha kocha wa Man United Jose Mourinho hatiani, kwani ndio zimezidi taarifa za kocha huyo kuwa atafukuzwa kazi na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane, hata hivyo Zidane ameripotiwa ameanza kujifunza tamaduni za waingereza kitu ambacho kinahusishwa kwa karibu na mpango wake wa kujiunga na Man United.

JB na Ray “Hata Yanga wao wanajua Simba ana timu bora”

By Jamhuri