Hali mbaya ya hewa inatatiza juhudi za kuzima moto na kufuja kwa mafuta zaidi ya saa sitini.
Meli ya mafuta ya Iran inateketea kwa moto baada ya meli mbili kugongana kusini mwa bahari ya China.
Meli hiyo kwa jina Sanchi imebeba tani 136,000 za mafuta.
Waokoaji sasa wamepanua shughuli ya utafutaji wa wahudumu 31 wa meli ambao hawajulikani waliko.
Ni mwili moja tu wa mhudumu kati ya wahudumu 30 raia wa Iran na wa Bangladesh wawili uliopatikana hadi sasa.
Raia 21 wa China waliokuwa kwenye meli ya mizigo waliokolewa.
Kuna hofu ya kutokea janga kubwa la kimazingira wakati meli hiyo inaendelea kufuja mafuta.
Katika taarifa leo Jumanne, wizara ya uchukuzi nchini China, ilisema upepo mkali, mvua na mawimbi yanaendelea kutatiza juhudi za uokoaji.

1524 Total Views 5 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!