Mamlaka ya kukabiliana na ufisadi nchini Zimbabwe imeanzisha uchunguzi kuhusu shahada ya udaktari iliopewa mkewe Robert Mugabe, Grace Mugabe kulingana na ripoti ya AFP.

Phyllis Chikundura ,msemaji wa tume ya kukabiiana na ufisadi nchini humo alithibitisha kuwa kulikuwa na uchunguzi uliokuwa ukiendelea.

”Tumethibitisha kuwa kuna ripoti kama hiyo na kwamba kuna uchunguzi kama huo pia”, alisema.

Bi Mugabe alidaiwa kupata Shahada hiyo baada ya miezi kadhaa ya masomo 2014.

Gazeti la serikali The Herald liliripoti wakati huo kwamba kutoweka kwa Bi Mugabe kulifanywa kwa lengo la kubadilisha hali ya jamii na kazi ya familia.

Inadaiwa kwamba alifanya utafiti kuhusu nyumba za watoto wa Zimbabwe.

Bi Mugabe yeye mwenyewe alituzwa shahada hiyo na aliyekuwa rais wa taifa hilo Robert Mugabe ambaye alikuwa chansela wa chuo kikuu cha Zimbabwe.

Alipongezwa wakati huo na maafisa wengine wa serikali waliotetea shahada hiyo yenye utata.

Bi Mugabe alitumai kumrithi mumewe kama kiongozi, lakini akachokoza upande mmoja wa chama cha Zanu-Pf ambacho hatua iliosababisha mgawanyiko ndani ya chama hicho.

Jeshi baadaye lilingilia kati na kumlazimisha rais Mugabe kuondoka madarakani baada ya kipindi cha miaka 37 na kumuweka mamlakani aliyekuwa makamu wake Emmerson Mnangagwa kuwa rais.

By Jamhuri