Wiki iliyopita makala hii iliishia kwa kueleza kuwa Palestina si makazi ya kihistoria ya Wayahudi. Mnamo 1920 baada ya suala la udhamini wa Uingereza kwa Palestina lilipojadiliwa na Bunge- The House of Lords, Lord Sydenham alitamka… Endelea.

 

“Naeleza kwa dhati ya moyo wangu juu ya utashi wa Wayahudi wa kuwa na nchi yao. Lakini nasema ya kwamba, nchi hiyo haipaswai kutwaliwa katika misingi ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Palestina siyo ardhi/ nchi ya awali ya Wayahudi. Ilitwaliwa na Wayahudi kwa njia za mabavu- na hawakuitwaa yote na kwa sasa wanaitaka hadharani/ bila kificho. Hawana uhalali  wa kuidai Palestina kuliko uzao wa Warumi- wa kale kwa nchi hii.”

Warumi waliikalia Uingereza kama tu ambavyo Waisraeli walivyoikalia Palestina. Kama tutakubaliana na madai ya ukaliaji wa eneo fulani wa miaka maelfu iliyopita, basi duni nzima ingekuwa “miguu juu kichwa chini”.

Jambo la pili, Wayahudi wa karne ya 20 ni wale waliohuishwa  kwenda kwenye Judaism- na hawana mahusiano ya kinasaba au kitabaka na Waisraeli .

 

AZIMIO LA BALFOUR:

Azimio la Balfour limekuwa likitegemewa na  Wanazayuni  kana kwamba  ulikuwa ni waraka wa hati  miliki ya Palestina. Kabla hatujachunguza uzito wa kisheria  wa Waraka ule, ni vema tukaangalia kwanza  mazingira  ambamo ulipatikana na maana yake halisi.

Mnamo 2 November, 1917, Arthur James Barfour, Waziri wa mambo ya nchi za  nje  wa Uingereza  akizungumza  yafuatayo  kwa Lord Rothsechild:

“Ninayo furaha kubwa kwa niaba ya serikali ya kifalme kuwasilisha azimio la matakwa ya Wayahudi wa Zayuni ambalo limewasilishwa na kuthibitishwa na Baraza la Mawaziri. Serikali ya kifalme inapendekeza uwanzishwaji  wa Taifa la Wayahudi ndani ya Palestina- na serikali itatumia kila juhudi kuhakikisha damira hii  inafanikiwa…”

Mawasiliano haya ambayo yalikuja kujulikana kama – Azimio la Balfour yalisababisha matatizo makubwa katika zama hizi. Matatizo ambayo yameichanganganya Mashariki ya Kati kwa zaidi ya miongo sita; na  ambayo  hata  leo hayajakoma kutikisa misingi ya ukanda husika. Azimio  hili liko katika mizizi  ya Janga la Palestina na mgogoro wa Waarabu na Israel.

Azimio la Balfour liliwakilisha mbinu na mikakati ya kunyakua uungwaji mkono wa Waingereza kwa ajili ya mpango wa kuitawala Palestina na kuanzisha dola ya kiyahudi. Mpango ule, awali uliasisiwa na Theodor Herzl  mnamo 1896 na ulitekelezwa kwa mara ya kwanza na chama cha Ki-zayuni (Zionist Congress) pale Balse mnamo 1897.

Wazayuni walisitisha ushiriki wa vita ya Kwanza vya Dunia kupata ungaji  mkono wa Waingereza kutimiza dhamira yao ya kutwaa Palelstina.

Rasimu ya tamko ilitayarishwa na Wazayuni na kuwasilishwa kwa Baraza la mawaziri la Serikali  ya Uingereza kwa ajili ya uthibitisho. Rasimu ya Wazayuni ilidokeza kutambuliwa kwa ardhi yote ya Palestina  kama makazi ya Wayahudi na serikali ya Uingereza- na kutotoa hakikisho la haki ya usalama kwa wakazi wa eneo lile.

Dhana ya kuifanya Palestina kuwa makazi ya Wayahudi ilipingwa na Wayahudi – Waingereza ambo japo walikuwa na huruma juu ya Mtakatifu wa   Jerusalem, wakipinga uhusishwaji wa fungate la kisiasa ndani ya Palestiina, ama kukasimiwa kwa haki maalum kwa Wayahudi dhidi ya jumuia mbalimbali zilizokuwa zikiishi Palestina.

Upinzani wao haukufua dafu dhidi ya mpango wa Wazayuni, lakini ilifanikisha kupunguza  kasi katika minajiri miwili.

i) Badala ya kuitambua Palestina kama nchi ya ahadi ya Wayahudi tamko lile lingezingatia kuangalia uwezekano wa upendeleo ule na;

ii) Hakikisho la usalama liliongezwa bayana ya kwamba “Hakuna ambacho kingefanyika chenye kuibua haki za kiraia na zile za kidini  dhiki ya jumuia mbalimbali ambazo si za Kiyahudi katika ardhi ya Palestina.

Ukweli ulio dhahiri – ya kwamba idadi ya Jumuia zisizokuwa za Kiyahudi ziliwakilisha 92% ya watu wote, haukuzuia Uingereza kutoa uungaji mkono kwa Wazayuni  katika kutimiza azma yao.

Wala serikali ya Uingereza haikutetereka katika msismamo wake licha ya kwamba- iliwahi kutoa hakikisho la awali na ahadi kedekede kwa Waarabu juu ya uhuru wao baada ya vita.

Je, unafahamu msimamo wa Uingereza uliadhirije usitawi wa mataifa haya mawili? Itaendelea wiki ijayo.

 

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa Anapatikana kwa:-

 (+255)784  142  137

(+255) 713 333141

Au  barua  pepe

ngayasteve@gmail.com

brilliantconsult2000@gmail.com

2661 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!