Mke wa Rais wa 41 wa Marekani, George HW Bush na maa wa Rais wa 43 wa nchi hiyo George W Bush amefariki dunia akiwa na umri wa miaka.

Barbara Bush, ambaye mume wake amekuwa rais tokea mwaka 1989 to 1993, alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu kabla ya kukutwa na umauti.

Barbara amekuwa mke wa Rais Bush na ndoa yao imedumu kwa miaka 73. Ni mwanamke wa pili katika historia ya Marekani kuwa na mume na kisha mtoto (George W. Bush) kama marais wa nchi hiyo.

Barbara Bush na George HW Bush wameishi katika ndoa kwa muda wa miaka 73

Barbara alikutana na aliyekuja kuwa mume wake George HW Bush kwa mara ya kwanza mwaka 1941 wakati wa sikukuu ya Krismasi, na mwezi Januari mwaka huu waliadhimisha kumbukumbu ya miaka 73 ya ndoa yao.

Katika ndoa yao walifanikiwa kupata watoto sita, japo mmoja wa kike aliyeitwa Robin, alifariki mwaka 1953 akiwa na umri wa miaka mitatu kutokana na ugonjwa wa Leukaemia.

Watoto wengine ni George, Jeb, Neil, Marvin na Dorothy.

1501 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!