Ngombale-Mwiru: Afisa JKT asiye na ‘rank’

Nimefurahishwa na ule ufafanuzi uliotolewa na Monsinyori Deogratias
Mbiku katika Gazeti la Kiongozi toleo No. 06 la tarehe 09 – 15
Februari 2018 uk. 3 – 4. Kwa maelezo yake katika “Gumzo kuhusu Kanisa
kumzika Kingunge” Monsinyori ameeleza wazi namna alivyoongea na
mgonjwa – Mzee Kingunge pale hospitalini Muhimbili.
Naamini wasomaji wengi wamekolezwa lile dukuduku lao na huenda
hawataendelea tena na udadisi wao eti kwa nini Kanisa lilimzika mzee
huyu ambaye hakuamini kuwa Mungu yupo na wala hakuwa na dini yoyote.
Monsinyori amedhihirisha hapa kuwa Mzee Kingunge alikuwa MKRISTO tena
siyo Mkristo tu, bali muumini wa madhehebu Katoliki. Mzee Kingunge
alibatizwa, akapokea Komunio, akapata Kipaimara, alifunga ndoa katika
Kanisa Katoliki Mivinjeni kwa Wabenediktine – wakati wa Padri Beda
Pavel OSB, na kabla ya kufariki dunia alipakwa mafuta ya wagonjwa na
yeye Monsinyori Mbiku pale Muhimbili. Hayo yamewekwa wazi. Ni neema za
Mungu hizo.
Wengine waliitwa saa 11 kwenda kufanya kazi katika shamba la Bwana kwa
ujira ule ule wa dinari moja kama wale walioanza (Mat. 20:8 – 9).
Basi, kwa vile hata mimi ninamfahamu Mzee Kingunge nimeona nijitokeze
kusema machache juu yake pia. Tulikutana katika Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT) Makao Makuu mwaka 1969. Mzee Ngombale-Mwiru baada ya kutoka
Algiers, Algeria alikokuwa akifanya kazi kama Katibu Mkuu wa Umoja wa
Vijana wa Afrika, Mwalimu Nyerere alimteua kuwa Mkuu wa Elimu ya Siasa
katika JKT mwaka 1968 yaani alikuwa KAMISAA katika JKT. Cheo kile kwa
kifupi kinaitwa CPEO kirefu chake ni Chief Political Education Officer
na anakuwa Makamu wa Mkuu JKT.
Mimi nilihamishwa kutoka Mafinga Januari 1969 kwenda Makao Makuu ya
JKT kuwa Msaidizi wake yaani kwa kijeshi ni 2 1/C wa CPEO. Tukawa
katika ofisi moja tangu hiyo 1969 Januari. Mzee Ngombale ndiye
aliyebuni mbinu ya kufundisha siasa kwa mtindo wa semina katika JKT.
Hapo aliimarisha ile Idara yetu ya Siasa kwa kuwaajiri (recruited)
Mwalimu Bonifas Njokole kutoka Chuo cha Kivukoni na Afisa Utawala,
Adam Mwakajuki, aliyekuwa Biharamulo kama Administrative Officer grade
VI tukawa na timu ya watu wanne katika idara yetu. Mwaka 1969 hiyo
ndipo JKT ikaanza kutumia ule mtindo wa kufunza siasa kwa semina.
Tulianza kambi la Mgulani, tukaenda Mafinga, Makutupora, Oljoro na
kumalizia Ruvu – wakati ule kulikuwa na Operation Ufundi. Mafunzo hayo
yalihusu viongozi wote wa JKT na katika CTS zote yaliyotolewa kwa
kuruta wote na viongozi wao.
Mwanzoni mwa 1970 kulizuka sintofahamu Makao Makuu ya JKT au niseme
sokomoko la kiutawala. Wakati ule Mkurugenzi wa JKT – alikuwa Robert
Shija Kaswende. Huyu alitaka kwenda likizo yake ya mwaka (annual
leave). Ilibidi kwa utaratibu wa kiserikali apendekeze wizarani jina
la afisa wa kukaimu ukuu wa JKT. Basi, mkuu kimadaraka alikuwa huyu
Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru, akifuatiwa na Assistant Director Laurent
M. Gama ambaye kwa wakati ule alikuwa School Leader wa Ruvu JKT.
Mzee Kaswende DNS, hakutaka kukabidhi madaraka kwa yeyote kati ya hawa
wawili. Alimpendekeza Master Uriel Mushi – akawaruka hao wakuu wawili.
Hapo basi Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Ofisi ya Makamu wa Pili
wa Rais akiitwa Bernard Mulokozi – Afisa mwenye kufuata sheria na
kanuni zote za utumishi serikalini (a very conversant officer with
rules and government regulations in civil service) akatupilia mbali
pendekezo la Mkuu wa JKT. Hapo ndipo sokomoko likaanza.
PS Bernard Mulokozi alikuja mwenyewe Makao Makuu ya JKT pale Garden
Avenue/Ohio siku hizi zipo Ofisi za Shirika la Simu (ATCL), moja kwa
moja akaingia ofisini mwangu na kusema; “Francis, Ngombale-Mwiru yuko
wapi? Kwa nini mpaka leo hii hakujibu barua ya Serikali offering him
his appointment?”
Mimi kwa hofu na mshangao nilisema tu kuwa CPEO kenda nyumbani
anauguliwa na mtoto wake. Hapo PS akanipa nakala ya “Appointment
letter” nimpelekee na maagizo kuwa Ngombale ajaze fomu zile na
azipeleke ofisini kwake kule Magogoni kabla ya saa 10 jioni. Akanipa
angalizo kuwa kutokutimiza yale maana yake hataki kazi serikalini!
Nakala ya format ya appointment letter ni hii naambatanisha hapa.

LETTER OF OFFER OF APPOINTMENT IN PERMANENT TERMS
MINISTRY OF DEFENCE AND NATIONAL SERVICE
OFFICE OF THE SECOND VICE PRESENT
P.O.BOX 3021
DAR ES SALAAM.

TO……………………………………..
…………………………………………
ufs……………………………………
……………………………………..
Ref. No. …………………………….
Sir/Madam,
I have pleasure in offering you appointment, on the advice of the
Public Service Commission as
…………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
Please arrange to forward your written acceptance of the terms of this
appointment endorsed on the annexure at the foot of this letter.
You are also requested to complete and return the following documents
which are enclosed
(i) Next of Kin Card (ii) Declarations regarding responsibility under
the official Secretes Ordinance and membership of Political
association.
Your appointment would take effect from ………………………………. Formal
confirmation of your appointment would be by publication in the
official Gazette.
I am, Sir,
Your obedient servant
……………………….
For Permanent Secretary
Copy to:
Principal Secretary, Public Service Commission, Dar es Salaam
Permanent Secretary to the Treasurer, Dar es Salaam
Mzee Ngombale hakuijibu barua ile ya mwaka 1968 na hivyo kusababisha
sokomoko la kiutawala katika JKT.
Nikaenda Oysterbay Mkwawa Road nyumbani kwa Ngombale nikamkabidhi
maagizo yale ya Katibu Mkuu wa Ulinzi.
Mzee Ngombale-Mwiru alishtuka sana na kuniuliza’ “Kwani vipi, bwana,
kuna tatizo ofisini?” Nikamwambia; “Afande ulipoajiriwa ulipewa barua
namna hii uijaze na kurudisha majibu kama umekubali appointment ile”.
Mzee Ngombale-Mwiru baada ya kutazama ile “letter of appointment”,
akaonekana kutokukumbuka akasema tu nadhani kweli nilipata, lakini
sikumbuki kujibu na wala sijui sasa niliweka sapi? Hapo nikamwambia
jaza hii ambatanisha na ripoti ya daktari na uipeleke kwa Mulokozi
kabla ya saa 9 leo hii.
Ninachokumbuka ni kuwa Mzee Ngombale alijisemea; “Haya mambo yenu ya
serikalini mie siyawezi bwana! Haya nisaidie kujaza.” Tukajaza,
akaenda Ocean Road kupata “Medical Report” na ilipofika saa 9 tukaenda
Magogoni, Ofisi ya Makamu wa Rais akarejesha barua yake kwa Bernard
Mulokozi PS Ulinzi na JKT ikiwa imesainiwa, lakini kwa tarehe za huko
nyuma 1968 (retrospective back dating).
Hapo Katibu Mkuu Ulinzi na JKT akamwambia Mzee Ngombale, ajifunze
kanuni na sheria za utawala serikalini – kutoka “GENERAL ORDERS na
CIVIL SERVICE REGULATIONS” kwa sababu yeye (Ngombale-Mwiru) ndiye
Makamu wa Mkurugenzi wa JKT kwa cheo chake kile cha CPEO (ni
Presidential Appointment ni Deputy Director of NS).
Baada ya siku tatu tu, Mzee Ngombale-Mwiru alipokea barua kutoka
Katibu Mkuu Utumishi (akiitwa David Mwakosya) ikimweleza kuwa alikuwa
tayari amethibitishwa katika kazi serikalini (confirmed officer).
Ndipo yule PS Ulinzi Bwana Bernard Mulokozi akamweleza Mkurugenzi
Kaswende akiwa bado anataka kwenda likizo yake ile ya mwaka sasa
amkabidhi madaraka ya JKT Mzee Kingunge CPEO ambaye ki-seniority ndiye
aliyestahili kukaimu maana ameshathibitishwa kazini.
Mkurugenzi Kaswende akatoa hoja kwa PS kuwa Mzee Ngombale-Mwiru
alikuwa RAIA na JKT ni Jeshi haliwezi kuongozwa na raia kwani hajui
MILA na DESTURI za Kijeshi wala havai “uniform” na hana “RANK” yoyote
ya kijeshi. Bado Kaswende aliomba amwachie madaraka Master Uriel Mushi
katika JKT ambaye ni mwanajeshi.
Kwa vile hoja ya Mkurugenzi ilikuwa halali hapo Katibu Mkuu Bernard
Mulokozi ambaye anajua sana General Orders na Civil Service
Regulations (very conversation with rules and regulations in Civil
Service), aling’ang’ania kuwa Master Mushi hangestahili kukaimu
madaraka ya DNS (Director of National Service) wakati CPEO na
Assistant Director NS walikuwa senior kwake. CPEO ndiyo huyo RAIA
Ngombale ADNS Gama ni School Leader wa Ruvu hapo ndipo ngoma ikawa
bado ngumu.
Wizara, kwa maana ya waziri mhusika ambaye alikuwa Mzee Rashid Kawawa
na Katibu wake Mkuu huyo Bernard Mulokozi wakatoa uamuzi kuwa Mzee
Ngombale-Mwiru aende kuhenya ulikruti Ruvu ili akihitimu alingane na
atakaowaongoza. Hapo likizo ya DNS Kanswende ilifutwa. Ndipo Mzee
Ngombale-Mwiru akaenda Ruvu mwezi Februari 1970 – OPERATION NGUMBARU
kwa mafunzo ya miezi mitatu, hadi Juni 1970.

ITAENDELEA….