Nyerere: Kiongozi hang’ang’anii ofisini

“Tuna viongozi wachache sana kwa maana halisi ya neno ‘kiongozi’, yaani ‘mwonyesha njia’. Huwezi kuonyesha njia kwa kung’ang’ania ofisini.”

 

Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyasema haya katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Taifa, Agosti 16, 1990, jijini Dar es Salaam.

Watson: Sitaki hofu ya kushindwa initawale

“Sitaki hofu ya kushindwa inizuie kufanya mambo ambayo kiuweli ninayajali na kuyathamini.”

 

Hii ni kauli ya msanii na mwanamitindo maarufu wa nchini Uingereza, Emma Watson.

 

Bagnasco: Kujitambua kunajenga kujiamini

“Kwa jinsi unavyoweza kujitambua uwezo na upungufu wako, ndivyo unavyojenga tabia ya kujiamini.”

 

Haya yalisemwa na Angelo Bagnasco, Askofu Mkuu wa Genoa na Rais wa Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Italia.

 

Michelle: Tuangalie milo ya familia zetu

“Sisi wote tunahitaji kuanza kufanya baadhi ya mabadiliko kuhusu jinsi gani familia zetu zinapaswa kula.”

 

Maneno haya ni ya Michelle Obama, Mke wa Rais wa 44 wa Marekani, Barack Obama.

1378 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!