Nyerere: Chama kisilazimishe watu kukichangia fedha

“Kwamwe chama [cha siasa] kisitoze kodi, au ushuru, au malipo ya nguvu-nguvu kwa mtu yeyote, awe mwanachama au si mwanachama. Michango yoyote ya fedha inayotolewa kwa ajili ya shughuli za chama lazima itokane na ridhaa ya mtoaji mwenyewe.”

Haya ni maneno ya Baba wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Indrawati: Mwanamke muhimu katika maendeleo kiuchumi

“Utafiti wa kina umeonesha kuwa mwanamke yuko katika mazingira magumu, lakini pia anao uwezo mkubwa wa kuongoza maendeleo ya kiuchumi.”

Hii ni kauli ya Sri Mulyani Indrawati, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia na Waziri wa Fedha mstaafu wa Indonesia.

 

Abdullah: Saudi Arabia siku hizi imebadilika

“Saudi Arabia pia imebadilika. Watu leo wanaunganika na kila mmoja kote duniani kwa njia za zana ndogo na televisheni. Ni jamii tofauti.”

Kauli hii ni ya Mfalme wa Saudi Arabia, Abdullah bin Abdulaziz al Saud. Alirithi wadhifa huo kutoka kwa kaka yake anayeitwa Mfalme Fahd.

 

Mengi: Wachimbaji wadogo wasaidiwe kiuchumi

“Naomba Korea Kusini ifikirie kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini hapa Tanzania waweze kuboresha shughuli zao na kuondokana na umaskini unaowakabili.”

Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni za IPP, Dk. Reginald Mengi, alitoa ombi hilo kupitia kwa Balozi wa Korea Kusini hapa Tanzania, Chung Il.

By Jamhuri